Na Woinde Shizza michuzi Tv,Arusha

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dkt Maulid Madeni leo amemsimamisha kazi Mkuu wa Idara ya Mipango Miji na Ardhi, Dickley Nyato na Ofisa Mipango Takwimu na Ufuatiliaji (Mchumi Wa jiji ), Anna Mwambene ili kupisha uchunguzi wa eneo la ujenzi kituo cha mabasi lililopo eneo la Bondeni City mkoani hapa lenye ukubwa wa ekari 30.

Akizungumza na Waandishi wa habari Novemba 25, 2019, Dkt Madeni amesema baada ya halmashauri kubaini ubadhirifu wa Sh1.9 bilioni za ununuzi wa eneo la ekari 29.5 lililopo Mtaa wa Oloresho Kata ya Olasiti na kukataa kulipa fidia, wananchi waliamua kutafuta ekari 30 za bure zilizopo eneo la Bondeni City katika Kata hiyo.

“Eneo hili lilifanyiwa tathimini huko nyuma na muhtasari uliandikwa Februari 24 mwaka 2017 ukitutaka tulipe fidia Sh.bilioni 1.1 lakini mwaka huo huo Machi 6 ukaandikwa muhtasari mwingine ukitaka tulipe Sh.bilioni 1.9 sasa mimi nikakataa na nakataa hadi mwisho nanasema hamna ela ambayo itatoka kwa ajili ya kulipa fidia bora hiyo pesa tuendelee kujenga madarasa ya magorofa watotowetu wasome,” akibainisha Madeni 

Alifafanua kuwa kutokana na mvutano huo, alifanya uchunguzi na kuwataka wakuu hao wa idara kumuandikia barua za kujieleza juu ya mamlaka ya kubadilisha maamuzi ya Baraza walikopata na kuongeza kiasi hicho cha fedha.

Akibainisha kuwa uthamini wa pili uliofanywa haukuwa na vigezo vyovyote vya kisheria,ikiwemo kupitishwa au kukaa kwa kikao cha madiwani cha kuizinisha kufanya tathimini upya ya Julia fidia katika eneo hilo

Kwamujibu wa Dtk Madeni, waliandika barua zao na kumpelekea Novemba 19, mwaka huu, lakini baada ya kuzisoma hakuridhika na sababu zao hivyo ameamua kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi dhidi yao.

"Mkuu wa Idara ya Mipango Miji na Ardhi, Dickley Nyato amedanganya Ofisi Yangu kwakusema kuwa kiwanja hicho ambacho halmashauri imepewa kwa ajili ya kujenga standi hakina hati miliki lakini tumefatilia tukakuta ,kiwanja hicho kina hati tangu mwaka 1949 na itaisha mwaka 2048 kwaiyo hati hii itadumu kwa miaka 99 bado mbele ,kwaiyo ndugu huyu alipotosha mamlaka ya juu kwa kusema hamna hati ya kiwanja hicho na halmashauri ilitakiwa ikichukuwe na ijigawie wenyewe na sio kupewa" alibainisha Madeni

Alisema kwa upande WaOfisa Mipango Takwimu na Ufuatiliaji (Mchumi Wa jiji ), Anna Mwambene aliondolewa majukumu yake hadi pale uchunguzi utakamilika,huku akibainisha kwa kipindi chote cha kupisha uchunguzi ataruhusiwa kutoka nje ya mkoa bila kutoka taarifa kwa mwajiri wake pili anatakiwa kila baada ya wiki mbili katika Siku ya ijumaa anatakiwa aripoti katika OFISI ya mwajiri wake ambaye ni mkurugenzi.
Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dkt Maulid Madeni  akiongea na waandishi Wa habari ofisini kwake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...