Jioni ya leo tarehe 16 Novemba, 2019 Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally amekutana na wananchi mbalimbali wenye changmoto  kutoka mikoa ya Arusha na Morogoro nyumbani kwake Jijini Dodoma.

Miongoni mwa wananchi aliokutana nao ni Mzee wa Karatu Bw. Shauri Gwandu ambapo pamoja na kueleza changamoto za migogoro ya ardhi  zilizokuwa zikimkabili na Katibu Mkuu kutoa  maelekezo kwa viongozi wa Chama na serikali mkoa wa Arusha kushughulikia. 

Katika mazungumzo hayo, Mzee huyo pia amepongeza na kukazia msimamo wa Chama Cha Mapinduzi wa kila mwanachama kijinunulia sare za chama kwa fedha zao wenyewe tofauti na awali ambapo sare za CCM zilikuwa zikigawiwa bure na wakati mwingine kuzua upendeleo.

Huu ni utaratibu wa Dkt. Bashiru kukutana na wananchi wenye changmoto mbalimbali wakati wowote na siku zote za wiki katika kutekeleza maelekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kwa kila kiongozi  kwa nafasi yake kukutana na wananchi, kuwasikiliza changamoto zao na kuzitafutia majawabu kwa wakati.

Imetolewa na;
Katibu wa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
Chama Cha Mapinduzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...