Waziri wa Mambo ya Ndani,Mhe. Kangi Lugola akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo suala la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Uhalifu na matumizi mabaya ya silaha na mitandao ya kijamii.
WIZARA
ya Mambo ya Ndani pamoja na Jeshi la Polisi wametoa onyo kali kwa watu
ambao watabainika kutaka kuvuruga mchakato wa uchaguzi wa Serikali za
mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 24 mwaka huu kwa kutoa lugha za
kuchonganisha au kupotosha.
Kwa
mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani imesema Jeshi la Polisi limejipanga
kukabiliana na wote ambao wanatarajia kufanya matukio ya uvunjifu wa
amani na kwamba mbali ya kutiwa nguvuni wajiandae kudumbukizwa kwenye
maji ya washawasha na si kumwagiwa maji hayo kama ilivyozoeleka.
Akizungumza
leo Novemba 2,mwaka 2019 jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Ndani
Kangi Lugola amesema kuwa ole wao wenye mipango ya kuvuruga uchaguzi
kwani watashughulikiwa na kwamba vyombo vya ulinzi vimejipanga vizuri.
"Kuna
watu wamekuwa na tabia ya kutoa lugha za kuchonganisha wananchi kwa
kisingizo cha kufanya kampeni wakati wa mikutano ya kampeni. Wale wenye
tabia ya kupotosha au kuvunja amani safari hii hawana nafasi,anayebisha
ajaribu hata sasa aone .Washawasha watamwagiwa na sio tu kumwagiwa bali
tutawatumbukiza katika maji yenyewe,"amesema Waziri Lugola.
Ameongeza
kuwa Polisi wameandaa mpango kazi kuhakikisha UCHAGUZI wa Serikali za
Mtaa unakwenda vizuri ,hivyo atakayethubutu kujaribu kuuvuruga atakiona
cha moto chini ya yeye(Waziri) , IGP Sirro na Rais Dk.John Magufuli
wamedhamiria kuhakikisha amani iliyopo nchini inaendelea kuwepo na
hakuna anaeweza kuivuruga kwa kigezo cha uchaguzi.
Wakati
huo huo Waziri Lugola amesema Jeshi la Polisi limejipanga vizuri
kushughulikia matatizo ya wananchi na kwamba ametoa maagizo kwa IGP
Sirro kuhakikisha makamanda wa Polisi katika Mikoa yote na Makamanda wa
Polisi wa Wilaya wanapanga ratiba ya kwenda kusikiliza kero za wananchi
na kuzifanyia kazi.
Amesema
katika ziara za viongozi wakuu wa nchi, wamekuwa wakipokea malalamiko
na hivyo wamekubaliana makamanda hao watoke na ameahidi kufuatilia
utendaji wao na wale ambao watafanya kazi kwa kusuasua wajiangalie kwani
hatawavumilia .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...