JUMLA ya Taasisi 418 zimeunganishwa kwemye Matumizi ya Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kieletroniki (TANePS).
Hayo
yamesemwa Novemba 11,2019 jijini Dar es Salaam na Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA), Mhandisi Leonard
Kapongo alipokuwa akielezea utekelezaji wa magizo ya Waziri wa Fedha,
Dk.Philip Mpango kuhusu mfumo wa TANePS.
Alisema wakat waziri
anatoa maagizo hayo taasisi nunuzi zilizokuwa zimeunganishwa zilikuwa
303 huku jumla ya wataalam wa nunuzi na tehama wapatao 924 walikuwa
wamepatiwa mafunzo.
"Kutokana na juhudi kubwa zilozofanyika hadi
kufikia leo hii Novemba 11, 2019 jumla ya taasisi 418 zimeunganishwa
huku idadi ya watalaam waliopatiwa mafunzo kutoka taasisi nunuzi
wakifikia 1,600. Hii inamaanisha kuna ongezeko la taasisi 115
zilizounganishwa toka siku tuliyopewa maagizo Septemba 28 mwaka huu,"
amesema Kapongo.
Mhandisi Kapongo amefafanua utaratibu wanaotumia
kwa sasa ni kuwa mara baada ya taasisi nunuzi kupatiwa mafunzo taasisi
zao huunganishwa kwenye mfumo na taasisi hizo huagizwa na PPRA kuanza
kuutumia mfumo wa TANePS kwa kuweka mipango yao ununuzi kama hatua ya
awali.
Ameongeza baada ya hapo kuendelea na kutekeleza michakato
yote ya ununuzi inayofuatia ikiwemo kuweka matangazo ya zabuni ili
wazabuni waweze kushiriki kwa njia ya kieletroniki na kwamba kati ya
taasisi 418 zilizounganishwa, taasisi 200 zimekwisha anza mfumo huo hadi
leo kwa kuwasilisha mipango ya ununuzi ya mwaka yenye jumla ya zabuni
11,343 zenye thamani takribani shilingi Trilioni 11.3.
"Kwa zile
taasisi za umma ambazo hazijaunganishwa kwenye mfumo huo, PPRA inatoa
mwito kwa taasisi hizo kudhuria mafunzo maalum yakutumia mfumo huu
yanayoendeshwa na PPRA.
Orodha ya taasisi hizo itawekwa kwenye tovuti ya PPRA yaani www.ppra.go.tz," amesema.
Mhandisi
Kapongo amesisitiza awamu ya mwisho ya mafunzo itazihusisha taasisi
hizo na yanatarajiwa kuanza Novemba 16 mwaka huu na kuendelea hadi
kufikia wiki ya pili ya Desemba na matarajio yao baada ya kukamilika kwa
awamu hiyo taasisi zote nunuzi zitakuwa zimeunganishwa kwenye mfumo wa
TANePS.
Hata hivyo amesema kwa upande wa taasisi nunuzi ambazo
zingependa kufanyiwa mafunzo maalum zinaweza kuwasilisha maombi PPRA kwa
ajili ya kupatiwa maelekezo zaidi kuhusu taratibu za utoaji wa mafunzo
hayo.
"Nirudie tena kutoa rai kwa wakuu wa taasisi nunuzi kuwa
matimizi ya mfumo wa TANePS ni ya lazima kwa sababu ni takwa la kosheria
na kanuni zake na sio suala la utashi wa taasisi. Hivyo sisi PPRA
hatutaishia kutoa mafunzo na kuziunganisha tu kwenye mfumo taasisi
nunuzi bali tutafuatilia kwa karibu kuhakikisha matumizi sahihi na
kamilifu ya mfumo, hatutasita kuchukua hatua stahiki," amesema.
Aidha,
ametoa mwito kwa watoa huduma mbalimbali, wazabuni na makandarasi wote
nchini kuchangamkia fursa ya kushiriki kwenye michakato ya zabuni kwa
kujisajili kwenye TANePS kupitia tovuti ya mfumo ambayo ni www.taneps.go.tz.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA),Mhandisi Leonard Kapongo akifafanua umuhimu wa kuanzishwa kwa mfumo huo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kielektroniki (TANePS) kwa Waandishi wa Habari jana jijini Dar es Salaam,ambapo alisema kuwa jumla ya Taasisi 418 zimeunganishwa kwemye Matumizi ya Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kieletroniki (TANePS) kati ya Taasisi 540.Pichani kulia ni Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali-Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James .
Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA),Balozi Dkt Matern Lumbanga akizungumza mbelee ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) jana jijini Dar,kwa kuishukuru Serikali kwa kuanzisha mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kielektroniki (TANePS),ambao utaongeza ufanisi ndani ya Serikali na kuongeza zaidi pato la Taifa katika mustakabali mzima wa kuwaletea Wananchi maendeleo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...