Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imekabidhi Pikipiki mpya mbili Kwa vyama viwili vya msingi vya Ruicho na Nyakatuntu vya Wilayani Karagwe na Kyerwa mwishoni mwa Wiki hii, katika Hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Chama cha Ushirika KDCU Wilayani Karagwe.

Awali katika salaam za Benki hiyo zilizotolewa na Meneja wa TADB Kanda ya Ziwa Ndg. Mike Granta kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Japhet Justine, amesema TADB kupitia mkopo inayotoa Kwa wakulima, imekuwa na mchango mkubwa wa maendeleo kwa Mkulima mmoja mmoja na pamoja na Vyama vya msingi, huku akiongeza kuwa mpaka sasa zaidi ya shilingi Bilioni 44 ambazo zimeingia katika mzunguko wa kiuchumi huku ikiwa shilingi Bilioni 34, kati ya pesa hizo zikiwa tayari zimelipwa kwa Wakulima wa Wilaya za Karagwe na Kyerwa.

Kupitia Hafla hiyo Meneja Granta amekabidhi Jumla ya Pikpiki mbili mpya zenye jumla ya thamani ya Shilingi Milioni Tano, Kwa Vyama vya Msingi vya Ruicho ( Karagwe) na Nyakantuntu (Kyerwa) ikiwa ni ahadi iliyotolewa hivi Karibuni na Mkurugenzi Mtendaji Japhet Justine alipofanya ziara yake Wilayani Karagwe. Sababu kubwa ikiwa Vyama hivyo kufanikisha zoezi la kuwashawishi na kuwaunganisha pamoja wanachama wao kwa asilimia kubwa kufungua akaunti katika Benki hiyo. 

Katika hatua nyingine Mgeni Rasmi katika hafla ya kukabidhi Pikipiki hizo Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akizungumza na Wakulima hao, alisema kwa Upande wa Serikali mpaka sasa hali ni shwari kwa msimu huu wa ukusanyaji wa kahawa, na Amani na Utulivu ni wa kutosha kulinganisha na msimu uliopita, hali iliyochangiwa na ulipaji wa malipo yote ya awali kwa wakulima wa zao hilo, na kwamba hakuna mkulima yeyote anayedai. 

Aidha Mhe. Gaguti ameongeza kuwa hakuna mnunuzi aliyezuiliwa kununua kahawa kutoka Kagera, Bali wanunuzi wa kahawa ya msimu huu kwa asilimia mia moja ni wanunuzi binafsi, na wale wachache wanaolalamika na kueneza uzushi ni wale ambao hawakukidhi vigezo vya kibiashara, na ndio sababu msimu huu umekuwa bora kuliko misimu iliyopita.
Pichani Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, akikabidhi Pikipiki Mbili Kwa Wakulima wa Vyama vya Msingi vya Ruicho na Nyakatuntu zenye thamani ya Shilingi Milioni tano
Pichani ni Ndg. Mike Granta, Meneja TADB kanda ya ziwa, akitoa salaamu kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Benki hiyo, katika hafla ya kukabidhi pikipiki Mbili mpya kwa wanachama wa vyama vya Msingi Ruicho na Nyakatuntu Wilayani Karagwe.
Pichani ni sehemu ya Wakulima na wanachama wakiendelea kufuatilia matukio mbalimbali kwenye Ukumbi wa Chama Kikuu cha Ushirika (KDCU), uliopo Kamahungu, Wilayani Karagwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...