Viongozi wa Serika ya Mtaa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wameapishwa leo Novemba 29,2019 katika ukumbi wa Urafiki Social Hall Ubungo,na kuahidi kufanya mabadiliko makubwa ya kimaendeleo katika mtaa wao ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuri, inayotaka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kufikia maendeleo ya uchumi wa kati.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa mtaa huo Dkt. Jonas Benedict Tiboroha mara baada ya kuapishwa.
Amesema kazi ya kuwatumikia wananchi wa tawi lake imeishaanza hivyo basi wategemee mabadiliko pamoja na maendeleo. Anawaomba ushirikiano kwani kupitia ushirikiano utaleta chachu ya maendeleo.
Pichani ni Uongozi mpya wa Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwenyekiti Dr. Jonas Tiboroha ( wa nne kutoka kushoto) pamoja na wajumbe wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...