Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

TUME ya Ushindani Tanzania (FCC) kwa kushirikiana na Mamlaka za EWURA, LATRA, PURA, FCT, TCAA, TCRA na TASAC wataadhimisha maadhimisho ya siku ya ushindani Duniani ambayo huadhimishwa Novemba 5 kila mwaka na mwaka huu itaenda sambamba  na kongamano litakalowakutanisha wadau na wananchi kwa malengo ya kuwajengea uwezo na ufahamu zaidi kuhusiana na maadhimisho hayo pamoja na shughuli zinazofanywa na Mamlaka hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa bodi ya ushindani nchini (FCC), Profesa. Humphrey Moshi amesema Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku ya ushindani tangu mwaka 2015 na kwa mwaka huu maadhimisho hayo yamekuja na kauli mbiu inayoendana na masuala ya kiushindani yanayojitokeza kote Duniani ya " Kuhakikisha Ushindani Madhubuti katika Ukuaji wa Dunia ya Kimtandao."

Amesema kuwa kilele cha maadhimisho hayo yatakayofanyika Desemba 5 na Waziri mwenye dhamana ya Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa atakuwa mgeni wa heshima.

Prof. Moshi amesema kuwa mitandao imekuwa ikikuza biashara kama ikitumiwa vizuri, "Biashara mtandao ni ile inayohusisha mabadilishano ya taarifa kupitia mtandao wa kompyuta, kimsingi ni jambo zuri kwa kuwa tafiti zinaonesha kuna masoko ya kutangaza bidhaa kwa urahisi hata kwa kuvuka mipaka ukilinganisha miaka iliyopita" ameeleza .

Vilevile amesema kuwa lazima jamii itambue fursa za masoko ya mtandao licha ya kuwepo na baadhi ya changamoto,lakini tume hiyo itaendelea kuhakikisha inawezesha masoko na kuwasiliana kwa urahisi, na hiyo ni pamoja na kuimarisha mifumo na uwezo wa biashara.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani nchini Godfrey Machimu amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatahusisha maonesho mbalimbali kutoka kwa wadau pamoja na kupata fursa ya kujua utendaji kazi wa Mamlaka hizo.

Machimu amesema kuwa Tume ya Ushindani kupitia maadhimisho hayo wanaamini italeta chachu katika kutatua changamoto za biashara mtandao zinazowakabili wananchi kote nchini.

Siku ya Ushindani Duniani imekuwa ikiadhimishwa na Mamlaka za ushindani Duniani kote kuanzia Mwaka 1980, wakati wa Umoja wa Mataifa uliporidhia na kukubaliana na kanuni za kuzuia mienendo potofu ya biashara.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Godfrey Machimu akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani),leo jijini Dar akieleza kuhusu tume hiyo   ikishirikiana na Mamlaka za EWURA, LATRA, PURA, FCT, TCAA, TCRA na TASAC wataadhimisha maadhimisho ya siku ya ushindani Duniani ambayo huadhimishwa Desemba  5 kila mwaka,ambapo mwaka huu itaenda sambamba na kongamano litakalowakutanisha wadau na wananchi kwa malengo ya kuwajengea uwezo na ufahamu zaidi kuhusiana na maadhimisho hayo pamoja na shughuli zinazofanywa na Mamlaka hizo.

 Mkurugenzi wa Utafiti na Muungano wa Makampuni na Urabishi Dkt. Allan Syril Mlulla akifafanua zaidi mbele ya Waandishi wa habari  namna maadhimisho hayo adhimu kwa Wadau yatakavyofanyika sambamba na kutoa elimu na kueleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Tume hiyo.
Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani Prof. Humphrey Moshi akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar, kuhusu namna Tanzania ilivyojiandaa kuadhimisha siku hiyo,amesema Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku ya ushindani tangu mwaka 2015 ,lakini kwa mwaka huu maadhimisho hayo yamekuja na kauli mbiu inayoendana na masuala ya kiushindani yanayojitokeza kote Duniani ya " Kuhakikisha Ushindani Madhubuti katika Ukuaji wa Dunia ya Kimtandao."
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo. Picha na Michuzi JR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...