NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
KAMATI ya Wabunge wanaojihusisha na mapambano dhidi ya ugonjwa wa
Kifua Kikuu (TB) na Ukimwi imesema changamoto ya inayowakabili watu
wanaougua ugonjwa huo lakini hawafikiwi na huduma za tiba imeishawishi
kukutana na viongozi wa dini zote nchini.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo wabunge walio kwenye mapambano ya TB Oscar
Mukasa amesema jijini Mwanza alipozungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na mkutano utakaowakutanisha viongozi wa dini mbalimbali
nchini ili kusaidia kusambaza elimu kwenye jamii.
Mkutano huo utakaofanyika Ijumaa jijini Mwanza, mgeni rasmi atakuwa
Spika wa Bunge, Job Ndugai, ambapo Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenister
Mhagama na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI),Seleman Jafo watashiriki.
Alisema idadi ya watu nchini, wanaougua ugonjwa wa TB nchini ni kubwa
huku changamoto yao kubwa ikiwa ni kutofikiwa na huduma za tiba.
“Ugonjwa wa TB ni tatizo kubwa la kiafya duniani,na hapa nchini watu
zaidi ya 60,000 wanaougua hawafikiwi na huduma za tiba, hivyo kama
hawapati matibabu jambo ambalo ni hatari kwa kuwa mtu mmoja anaweza
kuambukiza watu 20,”alisema
Mukasa alisema wameamua kushirikisha viongozi wa dini kueneza elimu
kuoitia nyumba za na endapo zitatumika vizuri zitasaidia kufikisha
ujumbe na kuleta ufahamu kwa jamii juu ya tatizo na watakuwa
wameunganisha nguvu pamoja na serikali yao.
“Kazi ya Bunge ni kuleta ushawishi, kuleta ustashi wa kisiasa na
kuisimamia serikali na hivyo kutumia nyumba za ibada ni mkakati wa
kuongeza elimu kwa jamii katika vita ya kupambana na TB kuhakikisha
jamii haiathiriwi ,kwa sababu kabla ya kutumia dawa watajua
unavyoambukiza,unatibiwaje lakini bila elimu itakuwa kazi
bure,”alisema Mukasa.
Alieleza kuwa ushawishi huo wa viongozi wa dini utaifanya serikali
kuendelea kuongeza nguvu kwenye vita hiyo kwa kuwa hayatengenishwi
na mifumo ya dini na wakiamua wanaweza kufikia maeneo mengi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela alisema maambukizi ya TB yako juu
kwani takwimu za 2018 zinaonyesha wagonjwa wa TB 4,640 sawa na
asilimia 6 wanatoka mkoani humu.
“Jambo hili ni kubwa lakini linazungumzwa juu juu, hivyo wataalamu
wabobezi watatusaidia kupata elimu na taarifa sahihi kwenye mkutano
huo wa wadau ili kupambana na tatizo hilo kwa umahiri na ufanisi
mkubwa,”alisema Mongela.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa wadau ili kuweka mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa Kifua kikuu (TB),utakaofanyika Ijumaa jijini humu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge walio kwenye mapambano ya ugonjwa wa Kifua kikuu (TB) Oscar Mukasa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu mkutano wao na viongozi wa dini ambapo mgeni rasmi atakuwa Spika wa Bunge Job Ndugai.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge walio kwenye mapambano ya ugonjwa wa Kifua kikuu (TB) Oscar Mukasa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Mjumbe wa kamati ya wabunge walio kwenye mapambano ya ugonjwa wa
kifua kikuu (TB) na na Ukimwi akielezea mikakati ya kamati hiyo ili
katika juhudi za kudhibiti ugonjwa huo nchini ambapo Ijumaa wiki
watakuna na viongozi wa dini zote nchini na Spika wa Bunge Job Ndugai
atakuwa mgeni rasmi wa mkutano huo.Picha zote na Baltazar Mashaka
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...