Balozi wa Korea Kusini nchini Tae Ick Cho akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliowakutanisha wadau na Wizara zinazoshughulikia masuala ya ardhi kutoka Korea na Tanzania ambapo Balozi Tae amesema kuwa ili kufanikiwa lazima teknolojia iwe silaha madhubuti, leo jijini Dar es Salaam.
1.viongozi mbalimbali wa kampuni kutoka Korea wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo ulilenga kupeana taarifa na uzoefu kuhusiana na teknolojia ya masuala ya ardhi, jijini Dar es Salaam.
Washiriki mbalimbali wakiwemo wanafunzi wakifuatilia mjadalo huo.
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
TEKNOLOJIA bora katika kukuza uchumi imeelezwa kuwa ndio silaha pekee ya kimaendeleo na yenye kuleta ushindani katika soko la dunia na hilo litafanikiwa kama taifa litajikita zaidi katika kuwekeza zaidi katika teknolojia ya sasa ambayo imeteka soko la dunia.
Akizungumza katika ufunguzi wa wa mkutano wa siku mbili wa wadau wa sekta ya Ardhi "Geospatial Information Road Show" uliowakutanisha wataalamu wa masuala ya ardhi kutoka nchini Korea na Tanzania; Balozi wa Korea nchini Tae Ick Cho amesema nchi hizo mbili zimekuwa na ushirikiano wa hali ya juu hasa katika masuala ya biashara zilizoruhusu kuvuka mipaka na hiyo yote ni kwa malengo ya kukuza uchumi baina ya nchi hizo mbili.
Balozi Tae Ick Cho amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa jukwaa la "Geospatial Information Road Show" malengo makuu ni pamoja na kuendesha semina za kiteknolojia katika usajili ardhi, mikutano ya biashara baina ya Serikali ya Tanzania Makampuni wakilishi ya Korea yaliyopo nchini pamoja na kupeana taarifa mbalimbali katika masuala ya ardhi.
Amesema kuwa ili kuendelea zaidi lazima teknolojia iwe silaha ya kwenda sambamba na maendeleo na bila teknolojia uwezo wa kushindana na mataifa mengine hautakuwepo.
"Matumizi ya teknolojia hasa ICT yana tija sana katika kuyafikia maendeleo na bila hiyo hatutaweza kushindana na mataifa mengine yenye teknolojia ya juu, tukumbuke msemo wa ukiona vyaelea ujue vimeundwa , hivyo hatuwezi kuendelea bila ya kuweka mbele teknolojia, kushirikiana na kuondoa vikwazo" amesema.
Vilevile amesema kuwa kama ilivyo Korea Kusini lazima watu wajue maeneo yao, ardhi yao na kuitumia katika shughuli za kimaendeleo na kueleza kuwa haba na haba hujaza kibaba hivyo ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili lazima udumishwe zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa upimaji na ramani kutoka Wizara ya Ardhi Hamdounny Masour amesema kupashana habari na kubadilishana uzoefu baina ya kampuni kutoka Korea na Tanzania ni moja katika ya hatua kubwa ambayo itasaidia nchi hizo mbili kufikia malengo.
Masour amesema kuwa kupitia mkutano huo wataendelea kudumisha ushirikiano huo pamoja na kupeana taarifa za kisekta katika masuala ya upimaji wa ardhi.
"Ushirikiano baina ya nchi hizo mbili umekuwa wa kindugu na kupitia Geospatial Information Road Show na Wizara ya Ardhi tutaendelea kupeana taarifa za kisekta ili kuweza kuyafikia maendeleo" ameeleza.
Mkutano huo uliodumu yangu 2013 umewakutanisha wadau kutoka Wizara ya Ardhi nchini pamoja na Wizara ya Ardhi, miundombinu na usafiri kutoka Korea pamoja na wataalamu mbalimbali yakiwemo makampuni makubwa 12 kutoka nchini Korea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...