Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Mhandisi Samson Mwela amewataka wahitimu wa VETA kuitumia vyema taaluma ya Tehama kujiajiri.

Akizungumza katika Mahafali ya Chuo cha VETA Kipawa leo, Mhandisi Mwela amesema kuwa Serikali imewekeza sana katika miundombinu ya Tehama ambapo asilimia 94 ya maeneo yanayokaliwa na watu yamefikiwa na miundombinu ya mawasiliano.

Amesema kuwa vijana waliohitimu katika Chuo hicho ambacho kinaendesha kozi ya Tehama wana fursa za kujiajiri kutokana na Mazingira wezeshi ya Serikali katika miundombinu.

Amewataka vijana kuchangamkia fursa hizo hasa kwa kuzingatia kuwa fursa kwenye sekta hiyo hazihitaji mtaji mkubwa kuweza kujiajiri na kuwasisitiza kuwa waadilifu katika kazi zao ili kuepuka Uhalifu kwa kutumia Tehama.

Mkuu wa Chuo cha VETA Kipawa Dickson Mkasanga amesema kuwa Chuo hicho kinaendelea kufanya tafiti na bunifu mbalimbali zinazolenga kutatua changamoto zinazoikabili jamii pamoja na kuchangia katika uchumi wa viwanda.

Jumla ya vijana 122 wamehitimu mafunzo chuoni hapo katika fani za Tehama, Elektroniki na Kompyuta kwa ngazi za Ufundi Stadi Daraja la pili, Daraja la Tatu, Diploma pamoja na kozi za muda mfupi 

 Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Mhandisi Samson Mwela akizungumza na wahitimu pamoja na wageni waalikwa kwenye Mahafali ya nane ya Chuo cha tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya vijana 122 wamehitimu mafunzo chuoni hapo katika fani za Tehama, Elektroniki na Kompyuta kwa ngazi za Ufundi Stadi Daraja la pili, Daraja la Tatu, Diploma pamoja na kozi za muda mfupi. 
 Mkuu wa Chuo Cha VETA Kipawa Dickson Mkasanga akizungumza na wahitimu pamoja na wageni waalikwa waliofika kwenye Mahafali ya nane ya Chuo cha tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mafunzo VETA Kanda ya Dar es Salaam  Florence Kapinga aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam akitoa salamu za mkurugenzi kwa wageni waalikwa na wahitimu waliofika kwenye Mahafali ya nane ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. 
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Tanzania, Fortunatus Muslim akizungumza kwenye kwenye Mahafali ya nane ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. 
 Mhitimu wa  Level 2 Electronic Chuo cha Tehama VETA Kipawa Anzamen Frank akisoma risala kwa mgeni rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Mhandisi Samson Mwela wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. 

  Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Mhandisi Samson Mwela  akiwakabidhi vyeti vya kuhitimu baadhi ya wahitimu katika fani za Tehama, Elektroniki na Kompyuta kwa ngazi za Ufundi Stadi Daraja la pili, Daraja la Tatu, Diploma pamoja na kozi za muda mfupi wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. 
 Mwakilishi  wa waajili  kutoka BSS Ibsulators Company Limited, Joseph Nsoza akizungumzia namna wanavyowapokea waajiliwa wapya katika kampuni hiyo pamoja na changamoto wanazipata kwa wafanyakazi wapya wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. 
 Mwakilishi wa wazazi wa wahitimu, Eliasi Yunusu akitoa neno kwa wahitimu wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. 
 Picha za pamoja
Baadhi ya wahitimu wakiwa kwenye maandamano ya kitaaluma wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. 
Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Mhandisi Samson Mwela  akiwa kwenye maandamano ya kitaaluma wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Chuo Cha VETA Kipawa Dickson Mkasanga .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...