WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WAPEWA SIKU SABA KUWASILISHA TAARIFA YA MIKOPO YAO



Charles James, Michuzi Blog

HALMASHAURI zilizochukua mikopo kutoka katika mabenki ya kibiashara na bado hawajazitumia wametakiwa kuzirejesha ndani ya wiki moja.

Pia Halmashauri ambazo zilichukua mikopo kwenye mabenki hayo zimetakiwa kuwasilisha taarifa zao kwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI ndani ya wiki moja na wote watakaokaidi watachukuliwa hatua.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo leo jijini Dodoma kwenye mkutano wake na wandishi wa habari huku pia akimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuhakikisha anafuatilia taarifa zote bila kupepesa macho.

Waziri Jafo amesema kuwa wale wote waliyochukua mikopo na hawajaanza kuitumia wairudishe haraka ipasavyo kwani Taasisi zote za Serikali zikiwemo mamlaka za Serikali za Mitaa hazitakiwi kuchukua mikopo kutoka mabenki ya kibiasha.

“Hayo ni maelekezo kutoka katika walaka wa Barua ya Katibu Mkuu Hazina barua ya tarehe 13 /12/2016 barua yenye kumbu kumbu namba CBC.155/233/01 kuwa taasisi zote za serikali na mamlaka za serikali hazipashi kuchukua mkopo kutoka benki za kibiashara” Ameeleza Mhe Jafo.

Ametoa onyo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote ambazo zitawasilisha taarifa ambazo siyo sahihi au mikopo yao kutokua na sura yenye mashiko na kusema kwamba watachukuliwa hatua.

Ametoa wito kwa wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanawasilisha taarifa sahihi kulingana na mikopo waliyochukua na wasijaribu kufanya udanganyifu wowote.

" Kama ikatokea taarifa ya halmashauri ikawa ba na mashaka halafu Mkurugenzi alishaondoka bado haiwapi uhalali wa mikopo hiyo, haya ni maagizo na wanapaswa kutekeleza," Amesema Waziri Jafo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo akizungumza na wandishi wa habari kuhusiana na agizo lililotolewa kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kuwasilisha taarifa ya mikopo waliyochukua kwenye mabenki ya kibiashara.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...