Mjumbe maalum na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amewasilisha ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe Uhuru Kenyatta juu ya masuala mbalimbali ya mashirikiano baina ya Nchi hizo mbili na Kimataifa.

Katika Ujumbe huo Tanzania imesema itaiunga mkono Kenya katika nafasi ya Kiti na Mjumbe asiyewakudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha mwaka 2021/2022.

Mara baada ya kukabidhi na kueleza ujumbe wa Rais Dkt Magufuli kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyata,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amepata fursa ya kushiriki katika uzinduzi wa ripoti ya Mpango wa kujenga umoja na mshikamano baina ya wakenya ujulikanao kama Building Bridge Initiative,ambapo amewataka wakenya kushikamana na kuziba mianya ya siasa za kikabila ili kuwa na Taifa moja kwa ajili ya maendeleo.

Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta kwa upande wake amesema Taifa hilo kwa miaka mingi limekuwa likiendeshwa wa siasa za kikabila jambo ambalo amesema halileti afya kwa ustawi wa Kenya kutokana na kuwa kila baada ya uchaguzi Taifa hilo huanza kutibu majeraha yaliyotokana na uchaguzi badala ya kuzingatia masuala ya maendeleo.

Rais Kenyatta amewataka wanasiasa wenzake kuacha siasa zinazochochea mgawanyiko na kuwataka kutumia fursa iliyojitokeza kupitia Building Bridge initiative kutoa maoni ya namna bora ya kufanya siasa za kistaarabu zisizochochea uhasama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...