Na Ripota Wetu, Michuzi Globu ya jamii

WAZIRI wa Fedha na mipango Dk. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu 20 kati ya 16623 waliopata alama za juu katika mafunzo ya kukidhi vigezo vya kimataifa vya masoko ya mitaji na dhamana.

Utolewaji wa tuzo hizo unatarajia kufanyika kesho Novemba 28 ,2019 katika Ukumbi wa Benki  kuu jijini Dar es Salaam .

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mtendaji Mkuu wa mamlaka ya mosoko ya mitaji na dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama .amefafanua kuwa mamlaka  hiyo ambayo itatoa tuzo hizo kesho pamoja na mambo mengine  inawajibu wa kuendeleza na kusimamia masoko ya mitaji ambayo ni sehemu  ya mfumo wa sekta ya Fedha unaowezesha upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu au Fedha za muda mrefu kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Mamlaka hiyo ina majukumu makubwa mawili ambayo yanawezesha kuendelea na kusimamia ili kuhakikisha kwamba yanaendeshwa kwa mujibu wa Sheria katika kutimiza wajibu wa kuendeleza mamlaka hiyo imetekeleza mambo majumumu makubwa  mawili.

"Moja tuliendesha shindano la wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu nchini ambapo tulitarajia kuwa nawashiriki wapatao 7000 lakini tumeweza kupata washiriki 16623 hivyo tumevuka lengo na kuweza kupata mafanikio asilimia 233.

"Haya ni mafanikio makubwa sana katika shindano hili, na hii imetokana na matumizi ya simu ambayo tuliweza kutumia teknolojia ambayo tulifanya utafiti tuliona nyezo inayotumiwa na wanafunzi wengi  vyuoni na katika taasisi za elimu  juu nchini hivyo shindano hili limepata mafanikuo makubwa na kesho tutatoa tuzo.kwamba kwa waliopata alama za." Amesema Mkama

Amesema katika Utoaji huo wa tuzo mshindi wa kwanza atapata Fedha tasilim shilingi milioni 1.8 na mshindi wa pili atapata shilingi 1.4 ambapo mshindi wa tatu atapata laki 8 ,na mshindi wa nne  shilingi 4 na washindi wengine 20 waliopata alama za juu watapata laki 2.5.vilevile watatakiwa kuziwekeza katika hisa ambazo za Kampuni zilizoorodheshwa katika soko la hisa Dar es Salaam.

Amesema vilevile  kutakuwa na hafla za kuwatunuku watendaji katika masoko ya mitaji ambao wanakidhi  viwango vya kimataifa kwa ajili ya kujiendesha katika masoko yeyote ulimwenguni.

Pia amesema kampuni zilizowezesha kununua na kuuza hisa kwenye soko la hisa ambao wanaita na kwamba ili uweze kupata leseni kutoka katika mamlaka moja wapo moja ya kigezo ni kuhakikisha kwamba unapata mafunzo ambayo yanakidhi vigezo vya kimataifa na hiyo ni katika kutekeleza itifaki ya soko la Jumuiya ya Afrika mashariki ambapo taasisi katika usimamizi wa masoko  ya mitaji katika ukanda Afrika Mashariki wamekubaliana kwamba wanatakiwa kuweza kukidhi viwango na vigenzo vya kimataifa.

Amesema mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana ili weza kuingia makubaliano ya ushirikiano na moja  taasisi ya kimataifa ya nchini uingereza ili kuweza kushirikiana  kutoa mafunzo hayo hivyo waliweza kutoa mafunzo kwa shiriki ambao sasa wanakidhi vigezo vya kimataifa.
  Mtendaji Mkuu wa mamlaka ya mosoko ya mitaji na dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar kuhusu mamlaka hiyo kutoa tuzo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu 20 kati ya 16623 waliopata alama za juu katika mafunzo ya kukidhi vigezo vya kimataifa vya masoko ya mitaji na dhamana,ambapo ameeleza kuwa  katika tukio hilo Mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Fedha na Mipangap Dkt Philip Mpango.
Mtendaji Mkuu wa mamlaka ya mosoko ya mitaji na dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama akitoa ufafanuzi zaidi mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar namna mamlaka hiyo  ilivyojipanga kutoa tuzo hizona kuongeza kuwa Mamlka hiyo inawajibu wa kuendeleza na kusimamia masoko ya mitaji ambayo ni sehemu  ya mfumo wa sekta ya Fedha unaowezesha upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu au Fedha za muda mrefu kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...