Na innocent Natai, Morogoro
Mahakama ya Wilaya ya Ifakara Mkoani Morogoro imemuhukumu
kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela au faini ya shilingi Milioni Mbili
pamoja na kuviteketeza viuatilifu kwa gharama zake mwenyewe, Mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Yerusalem Mwamaja miaka 49 (Mhehe) baada ya
kupatikana na hatia ya kupatikana na viuatiliafu visivyo sajiliwa
Hukumu hiyo imetolewa Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Binge Njaga
Mashabara, baada ya kujiridhisha na hoja za mashahidi watatu wa upande mshtaka,
bila kuacha shaka yeyote.
Hakimu Mashabara
alisema vitendo kama hivyo vinawasababishia hasara wakulima na seikali kwa
ujumla ukiachilia mbali kuendelea kusababisha madhara kwa mazingira na kwa Afya
za binadamu wanyama na mimea. Hivyo alitoa adhabu hiyo ili iwe onyo na
fundisho kwa wote wenye tabia kama hizo.
Awali, Wakili wa
Serikali, alidai kuwa hakukuwa na kumbukumbu za mashtaka ya nyuma dhidi ya
mshatakiwa na hivyo kuiomba Mahakama kutoa adhabu kali ili iwe onyo na fundisho
kwa wote wenye tabia kama hizo.
Katika utetezi
wake Yerusalem Mwamaja alikubali mashtaka na aliomba apunguziwe
adhabu kwani ni mara yake ya kwanza kufanya kitendo hicho na hata rudia.
Akizungumzia hukumu
hiyo baada ya kutoka Mahakamani hapo Bw Solomon Shedrack Mungure amabaye ni
Mkurugenzi wa Viuatilifu kutoka ofisi ya TPRI Dar es Saalam ameipongeza
Mahakama hiyo kwa adahabu iliyotoa kwani itakuwa ni fundisho kwa wengine wenye
tabia za kufanya biashara za viuatilifu visivyo Sajiliwa.
Aidha ametoa rai kwa
wauzaji na wasambazaji wa Viuatilifu nchi nzima wenye tabia za kuuza na
kusambaza viuatilifu visivyo sajiliwa na kukaguliwa na TPRI kuacha mara moja
kwani zoezi la ukaguzi na kuwabaini watu kama hao halikomi ni la kila siku na
kila saa hivyo watakamatwa mara moja na kuwafikisha mahakamani.
Aidha amehitimisha
kwa kusema kuwa kuuza au kusambaza viuatilifu bila kwa na elimu pia ni kosa
kwani kunaweza kumsababishia madhara msambazaji au muuzaji wakati wa ufanyaji
biashara bila kuwa na elimu ya namna bora na salama ya kufanya biahara hiyo,
hivyo ni vyema wasio na taaluma hiyo kuacha kufanya biashara hizo mara moja na
wafuate kanuni na taratibu za kupata mafunzo na kibali cha kufanya biashara
hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...