Uzio wa Bandari ya Nyamirembe ukiwa umeshakamilika kama sehemu ya kuimarisha usalama bandarini hapo baada ya ujenzi wa miundombinu yake kukamilika.
 Baadhi ya nyumba za zamani ambazo zilikuwa zinatumiwa na watumishi wa Bandari ya Nyamirembe wilayani Chato mkoani Geita.
 aadhi ya mafundi wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa kuhusu ujenzi wa bandari ya Nyamirembe kutoka kwa Meneja wa TPA Bandari za Ziwa Victoria Morric Mchindiuza (PICHA ZOTE NA SAIDI MWISHEHE-CHATO)
 Baadhi
 ya mafundi wakiendelea na ujenzi wa gati lililojengwa katika bandari ya
 Nyamirembe wilayani Chato ikiwa ni mkakati wa Mamlaka ya Usimamizi wa 
Bandari(TPA) kuboresha miundombinu ya ya bandari za Viwa Victoria
 Muonekano
 wa gati ya Bandari ya Nyamirembe wilayani Chato ambapo ujenzi wake 
umekamilika kwa asilimia 100 awamu ya kwanza na mkakati wa Mamlaka ya 
Bandari ni kuanza ujenzi wa awamu ya pili ya gati hiyo ili kuosogeza 
kwenye kina kirefu cha maji kwa ajili ya meli kubwa kuweza kushusha na 
kupakia abiria pampoja na mizigo.
 Mafundi wakiendelea na ujenzi wa gati ya Bandari ya Nyamirembe ambayo tayari imekamilika kwa awamu ya kwanza.
 Sehemu ya muonekano wa gati ya Bandari ya Nyamirembe baada ya kukamilika kwa ujenzi wake.
 Mhandisi
 Anderson Robert Ndogae akizungumza waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa
 gati ya Nyamirembe wilayani Chato mkoani Geita.
 Moja
 ya jengo la Bandari ya Nyamirembe likiwa limekamilika ikiwa ni mkakati 
wa ujenzi wa miundombinu katika bandari hiyo kwa ajili ya kuboresha 
usafiri wa meli Ziwa Victoria.
Said
Mwishehe Michuzi Globu ya jamii -Chato
IMEELEZWA
kwamba hatua ya Mamlaka ya Usimami Iwa Bandari Tanzania (TPA), kukamilisha ujenzi
wa Bandari ya Nyamirembe wilayani Chato mkoani Geita, sasa kutafungua milango
ya usafirishaji wa mzigo na shughuli za utalii nchini. 
Pia
imeelezwa bandari hiyo itakapokamilika itakuwa ni uwezo wa kusafirisha mizigo
katika nchi za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
kuanzia Machi mwaka 2020 baada ya kukamilika kwa meli zinazoendelea kujengwa na
nyingine kufanyiwa matengeneza makubwa katika Ziwa Victoria. 
Hayo
yameelezwa na Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria Morris Machindiuza alipokuwa
akielezea hatua za ujenzi wa bandari hiyo ambapo tayari baadhi ya majengo
yamekamilika huku awamu ya kwanza ya gati nayo ikiwa imeshamilika licha ya
kuwepo kwa awamu ya pili ya ujenzi wa gati hiyo ili kuosegeza kwenye kina
kirefu cha maji kwa ajili ya meli kubwa kuweza kushusha na kupakia mizigio na
abiria.
Amefafanua
kuwa Bandari ya Nyamirembe ni mlago muhimu kwa uchumi wa Ziwa Victoria kwani
kwa muda mrefu ilikuwa na manufaa kwa wananchi na wasafirishaji wa mizigo na
kuchochea maendeleo huku akisisitiza kuwa bandari hiyo ni muhimu kwa TPA na
wananchhi kwa ujumla hasa.
"Historia
ya Bandari ya Nyamirembe ni kwamba ilianza kufanyakazi mwaka 1960 na tangu
wakati huo ilikuwa chini ya Shirika la Reli Tanzania(TRC).Hata hivyo kutokana
na mabadiliko ilipofika mwaka 1997 ilikabidhiwa kwa Kampuni ya Huduma za  Meli na tangu wakati huo zipo meli zilikuwa
zikifika hapa na kutia nanga na ambayo ilikuwa na uwezo wa kuibeba abiria 593
na kuibeba tani 350,"amesema.
Ameongeza
kuwa na meli hiyo ilikuwa ikibeba mazao mbalimbali yakiwamo ya pamba, mchele na
kwamba  ilikuwa kama daladala katika
maeneo yote muhimu ilikuwa inasimama kuchukua abiria na mizigo. "Na sasa
TPA kutokana na umuhimu wake tuliwekeza na kuiuhisha kwa kuanza ukarabati wake
kwa gharama za za Shilingi bilioni 4.128 kwa kuhusisha ujenzi wa gati,mnara wa
meli na  jengo la abiria.
Mchiundaza
amesema kuwa bandari hiyo sasa itakwenda kuchochea utalii na hiyo inatoka na
uwepo wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato, Rubondo ambapo pia shughuli za
utalii zitaongezeka.
 "Tuna matarajio makubwa ya kuongezeka kwa
watalii ambao watakuja kwenye hifadhi yetu mpya ya Burigi -Chato, hivyo kwetu
sisi TPA ni fursa nyingine ya kibiashara kwani wengi watapenda kutumia usafiri
wa meli kuja huku na kwa kukumbusha tu kusafiri kwa meli nako ni sehemu ya
utalii na wengi watapenda."
Mwisho
 


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...