WAKALA ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wanawakaribisha katika maonesho ya nne (4) ya Viwanda yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salama .

Akizungumza na michuzi Blog Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Loy Mhando amesema usajili wa makampuni, majina ya biashara, alama za biashara na huduma hataza pamoja na leseni za viwanda zinapatikana katika viwanja vya sabasaba ambapo maonesho ya bishara za viwanda yanafanyika.

Loy amesema leseni za biashara za kundi A nazo zinapatikana katika maonesho hayo hivyo wananchi wote wenye mpango wa kuanzisha biashara wafike katika viwanja hivyo ili wakapate huduma hiyo kwa urahisi zaidi na bila kupoteza muda.

Natoa rai kwa watanzania wote, wadau wote wa biashara na viwanda pamoja na wawekezaji wanaohitaji huduma zinazotolewa na BRELA kufika katika viwanja vya sabasaba kwa ajili ya kuangalia bidhaa zinazotengenezwa pamoja na kujipatia huduma mbalimbali zinazotolewa katika maonesho hayo". Amesema Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu (BRELA), Loy Mhando.

Hata hivyo Afisa Leseni za viwanda kutoka BRELA, Yusuph Nakapala amesema kuwa katika maonesho hayo utapata huduma ya kufanya usajili na kurasimisha biashara yako kwa njia ya mtandao na kupata cheti chako papo kwa papo.

Kwa upande wake Afisa Habari na Mawasiliano kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Robertha Makinda amewakaribisha wananchi kwa ujumla katika maonesho ya Nne (4) ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaama ili waweze kufanya usajili na kurasimisha biashara zao.

Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inawakaribisha wote kutembelea Banda lao  lililopo katika ukumbi wa Karume, banda namba 105 katika viwanja vya Mwl. J. K. Nyerere (sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa mtendaji Mkuu wa  Wakala ya usajili wa biashara na leseni (BRELA), Loy Muhando  watatu kutoka kulia akiwa na wafanyakazi wa BRELA pamoja na mteja ambaye amepata cheti cha jina la biashara papo kwa hapo baada ya kufanya usajili.
 Picha ya pamoja katika maonesho ya nne ya idhaa za viowanda yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Leseni za viwanda kutoka  wakala ya usajili wa biashara na leseni (BRELA), Yusuph Nakapala akizungumza na mteje aliyetembelea katika banda lao katika maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 
 Mteja akipata maelekezo jinsi ya kusajili biashara katika maonesho ya viwana yanayoendelea katika viwanja vya saasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari na Mawasiliano kutoka wakala wa usajili wa biashara na leseni(BRELA), Robertha Makinda Katikati akizungumza katika maonesho ya viwanda yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...