
Msanii wa muziki nchini Tanzania Said Juma Hassan almaarufu 'Chege Chigunda' amefunguka kuhusu maisha yao ya muziki kati yake yeye na msanii mwenzake Zuwena Mohamedi (Shilole).
Chege amesema, Shilole ni mpambanaji na anafanya kazi kwa bidii hategemei pesa zinazotokana na muziki ndio maana anajihusisha na mambo mengine.
Ameeleza kuwa, yeye na Shilole hawana miaka mingi tangia wawe na urafiki wa karibu na imetokea kuelewana Sana hususani katika kazi ambayo ni muziki na kusaidiana kwenye mambo mbalimbali ya kijamii
Pia , Chege amesema hawajawahi kufanya kazi ya pamoja ya kimuziki ambapo ni kwa sababu wanajali sana masuala mengine kama familia, ushauri wa kazi na sio kuwekeza nguvu nyingi katika kufanya nyimbo ya pamoja Cha msingi kwao ni uzima.
"Nampenda Shilole na yeye pia ananipenda japo upendo wetu sio wa kufanya nyimbo ya pamoja bali ni kushauriana ni nini kifanyike katika suala la muziki na huwa Shilole ananiambiaga kabisa kwamba Chege hii nyimbo hapana unatakiwa uifanye hivi na sio hivi. Ni msema ukweli, mshauri na hafichi kitu juu yangu,"amesema Chege
Katika yote hayo amesema ya kwamba miongoni mwa nyimbo alizowahi kushauriwa na Shilole ni Pombe, Waache waowane, Sweet sweet na alikuwa ni miongoni ya watu wa kwanza kabisa kuwasikilizisha nyimbo zake kabla hazijatoka au akitaka kuzitoa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...