Na Collins Ndanzi,Michuzi Globu,DSJ
Msanii wa mziki wa Hip-hop kutoka kundi la Weusi, Gnako amemkaribisha nchini msanii wa mziki wa reggae kutoka nchini Jamaica Debbie DeFire(62) kwa ajili ya kujiandaa na tamasha la Reggae litakalofanyika nchini Kenya.
Tamasha hilo litakalowakutanisha wasanii mbalimbali litafanyika nchini humo Desemba 26 mwaka huu.
DeFire ameshawahi kufanya kazi na wasanii wakubwa duniani wakiwemo msanii wa jazz kutoka Africa Kusini Hugh Masekela na wengine wengi.
Gnako amesema, DeFire ameshafanya kazi na wasanii wengi duniani wakubwa ila zaidi amefurahi sana kufanya kolabo na msanii mkubwa.
Wasanii hao wamefanya wimbo ujulikanao kama Bongo Land ambayo wawili hao wameshauanya ukiwa unaeleza juu ya uasili wa nchi ya Tanzania.
"Ni mtu ambaye amefanya kazi na Bob, na leo amefanya kazi na mimi, sichukulii poa hata kidogo ndo maana unaona nasisitiza kufanya interview kama hizi ili watu wamfahamu” amesema G nako katika mmoja ya mahojiano aliyoyafanya akiwa pamoja na Debbie.
Amesema, DeFire ni muimbaji na mtunzi wa nyimbo zenge mdondoko wa reggae,amewahi kutamba katika enzi ya miaka ya 1970 ambapo na vibao mbalimabili ikiwemo “Travelling” iliyosimamiwa chini ya dub music Pioneer baadae aliibuka na ngoma nyigine “Scratch” na “Uptown Rankin”.
"DeFire aliweza kuteka nyoyo za mashabiki enzi hizo kutokana na umahiri wake wa kuweza kutunga nyimbo na kuburudisha mashabiki wake akiwa jukwaani,"
DeFire alihamia jiji la Chicago nchini Marekani na kwa sasa anashikilia jina la “Chicago’s Queen of Reggae”.
Debbie yuko nchini Tanzania kwa ajili ya likizo na tamasha la reggae ambalo litafanyika nchini Kenya mnamo 26/12/2019.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...