Waziri wa Uwekezaji wa Tanzania,
Mhe. Angellah Kairuki (wa pili kulia kwa waliosimama kwa nyuma), Waziri
wa Uratibu wa Masuala ya Bahari na Uwekezaji wa Indonesia, Mhe. Luhut
Binsar Panjaitan (wa pili kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini
Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau (wa kwanza kulia) wakishuhudia utiaji saini
wa makubaliano ya awali ya ujenzi wa Hoteli yenye hadhi ya Nyota tano
Jijini Dodoma baina ya Kampuni ya PT Wijaya Karya (WIKA)ya Indonesia na
Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA-Afrika) mapema leo tarehe 17
Desemba, 2019 Jijini Dar es Salaam. Wanaosaini makubaliano hayo ni
Mtendaji Mkuu wa WIKA Bw. Destiawan Simeon (kushoto) na Katibu Msaidizi
wa CPA Afrika Bw. Said Yakubu.


Katibu Msaidizi wa Chama cha
Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA Afrika) Bw. Said Yakubu (kulia)
akibadilishana nyaraka na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PT Wijaya Karya
(WIKA)ya Indonesia Bw. Destiawan Simeon (kushoto) mara baada ya kusaini
makubaliano ya awali ya ujenzi wa Hoteli yenye hadhi ya Nyota tano
Jijini Dodoma. Utiaji saini wa makubaliano hayo yalishuhudiwa na Waziri
wa Uwekezaji wa Tanzania, Mhe. Angellah Kairuki (wa pili kulia), Waziri
wa Uratibu wa Masuala ya Bahari na Uwekezaji wa Indonesia, Mhe. Luhut
Binsar Panjaitan (wa pili kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini
Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau (wa kwanza kulia) waliosimama kwa nyuma.

Waziri wa Uwekezaji wa Tanzania,
Mhe. Angellah Kairuki (wa pili kulia) akizungumza na Waziri wa Uratibu
wa Masuala ya Bahari na Uwekezaji wa Indonesia, Mhe. Luhut Binsar
Panjaitan walipokutana kwa ajili ya kushuhudia utiaji saini wa
makubaliano mbalimbali ya uwekezaji Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Uratibu wa Masuala ya
Bahari na Uwekezaji wa Indonesia, Mhe. Luhut Binsar Panjaitan (katikati)
akizungumza na Waziri wa Uwekezaji wa Tanzania, Mhe. Angellah Kairuki
wakati walipokutana kwa ajili kushuhudia utiaji saini makubaliano
mbalimbali ya uwekezaji Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA BUNGE
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...