Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akiwa kwenye kikao chake
na Bodi/Menejimenti ya TANESCO kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na kulia kwake ni
Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi.

Waziri wa
Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akiwa kwenye kikao chake na
Bodi/Menejimenti ya TANESCO kilichofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto
kwake ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na kulia kwake ni
Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi.

Naibu Waziri
wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto), Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi
Innocent Luoga (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito
Mwinuka wakiwa kwenye kikao cha uongozi wa Wizara ya Nishati na Bodi na
Menejimenti ya TANESCO kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya
Wajumbe wa Bodi ya TANESCO, wakiwa kwenye kikao cha uongozi wa Wizara ya
Nishati na Bodi hiyo pamoja na Menejimenti ya TANESCO kilichofanyika
jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Kamishna Msaidizi wa
Umeme, Mhandisi Innocent Luoga wakiwa kwenye kikao chao na Bodi na
Menejimenti ya TANESCO kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………….
Waziri wa Nishati, Dkt Medard
Kalemani ameiagiza Bodi na Menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) kuhakikisha kuwa wanafanya tafiti kubaini vyanzo vipya vya
uzalishaji umeme ili kuongeza kiasi cha nishati hiyo nchini na kuweza
kufikia lengo la kuwa na megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025.
Dkt.Kalemani alitoa agizo hilo
tarehe 19 Disemba, 2019 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kati ya
Wizara ya Nishati na Bodi/Menejimenti ya TANESCO ambapo kikao hicho
kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Kamishna
Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga.
“Lazima tufanye tafiti kubaini
vyanzo mbalimbali vya kuzalisha umeme ukiacha hivi vilivyopo, hata kama
tusipotekeleza leo, vizazi vijavyo vitatekeleza miradi hiyo, mfano
tafiti za mradi wa umeme wa Julius Nyerere (MW 2115) zilifanyika miaka
mingi iliyopita, lakini mradi tunautekeleza sasa, hivyo nasi hatuna budi
kuibua vyanzo vingine.” Alisema
Aidha, Dkt Kalemani aliiagiza
Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuhakikisha kuwa maeneo yote nchini
yanaunganishwa na umeme wa Gridi ifikapo mwezi Juni 2022 ili wananchi
wapate umeme wa uhakika na pia Serikali kuokoa fedha zinazotumika
kununulia Mafuta ili kuendesha mitambo ya umeme kwenye baadhi ya maeneo
nchini.
Kuhusu kazi ya usambazaji umeme
vijijini, alisisitiza kuwa lengo la Serikali ni kufikisha umeme kwenye
vijiji vyote ifikapo mwezi Juni mwaka 2021 na asilimia 85 ya wananchi
wanapata umeme hivyo TANESCO ina jukumu la kuhakikisha kuwa lengo hilo
linafanikiwa.
Vilevile, Dkt Kalemani aliiagiza
TANESCO kuhakikisha kuwa, kila kiwanda au Taasisi ya umma inapojengwa,
inafikishiwa umeme lengo likiwa ni kuongeza mapato ya Shirika na pia
kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii nchini.
Aidha, aliiagiza Bodi na
Menejimenti ya TANESCO kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Shirika kutoka
shilingi Bilioni 46 zinazokusanywa sasa kwa wiki hadi kufikia Bilioni 52
kwa Wiki.
Dkt. Kalemani aliongeza kuwa,
Shirika hilo pia linapaswa kumaliza madeni yake ifikapo mwaka 2026,
linaboresha nidhamu ya watumishi ili kuweza kutoa huduma bora kwa
wananchi na kuhakikisha kunakuwa na mpango wa ukarabati wa miundombinu
ya umeme kwenye maeneo yote nchini.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa
Nishati, Subira Mgalu, pamoja na kuipongeza TANESCO kwa majukumu
mbalimbali wanayofanya, aliiagiza Bodi kujielekeza pia kwenye ukusanyaji
wa madeni ya TANESCO kutoka kwa wateja mbalimbali zikiwemo Taasisi za
umma kwani fedha zitakazopatikana zitasaidia Shirika kuweza kutekeleza
majukumu yake ipasavyo.
Aidha, aliiagiza TANESCO
kuangalia suala la malipo ya huduma ya umeme ili kuwe na utaratibu wa
malipo hayo kufanyika kwa awamu ili kuweza kuunganishia umeme wananchi
wengi zaidi na hivyo miradi hiyo ya umeme kuleta tija.
Kamishna Msaidizi wa Umeme,
Mhandisi Innocent Luoga, alisema kuwa, hali ya umeme nchini imeimarika
hivyo TANESCO inapaswa kujikita pia kwenye kazi ya kuongeza wateja wa
nishati hiyo ili kuongeza mapato.
Vilevile, alisisitiza kuhusu
suala la mikoa yote nchini kuunganishwa na gridi ya Taifa ili kuimarisha
hali ya umeme kwenye mikoa hiyo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...