Na.Khadija Seif, Michuzi TV.

MSHINDI wa mashindano ya kusaka vipaji (BSS) kujulikana mkesha wa krismas mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark Production Rita paulsen amesema kuwa mchakato wa kusaka vipaji kwa msimu wa 10 ulikua na changamoto mbalimbali ikiwemo washiriki wote walikua na sifa ya kuingia kambini .

"Washiriki 45 Bora ambao walipita kwenye mchujo walifanikiwa kuingia kambini Mikocheni jijini Dar es salaam na mchujo mwengine wa kila wiki uliendelea nakufanikiwa kupata washiriki 13 na mpaka Sasa tumebakiwa na washiriki wa 5 ambao wametinga fainali rasmi.

Aidha,Madam amefafanua zawadi ya Mshindi atakaeibuka kidedea kwa mwaka huu.

“Mshindi wetu atapewa zawadi nono yenye thamani ya shilingi milioni 50 za kitanzania ambao milioni 20 atapewa mkataba wa kurekodi na kusimamiwa kazi zake zote za muziki kwa mwaka mzima.







Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark Production Rita paulsen akizungumza na waandishi wahabari kuelekea fainali ya msimu wa 10 wa Mashindano ya Bongo star search (BSS) jijini Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...