KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Iringa Juma Bwire amesema Jeshi la Polisi mkoani hapa limejipanga vema kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa kutosha katika kipindi cha Sikuu ya Krismass na mwaka mpya huku akitoa rai kwa wananchi kujiepusha na ulevi wa kupindua, kuendesha vyombo vya usafiri wakiwa wamelewa pamoja na kupiga marufuku disko toto.

Akizungumza leo Desemba 24, mwaka 2019 , Kamanda Juma Bwire amesema jeshi hilo limeimarisha ulinzi wa kutosha na kila kona ya mkoa huo hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi wakati huu wa kuherehekea sikuu za Krismass na mwaka mpya.

Amefafanua kuwa wananchi wa Mkoa wa Iringa kwa mwaka huu wa 2019 wamekuwa na ushirikiano mzuri na jeshi la polisi, hivyo kusaidia kunguza matukio ya uhalifu na kuufanya mkoa kuwa salama, hivyo ni vema wakaumaliza mwaka salama na kuanza mwaka mpya wa 2020 salama.

Kamanda Bwire amesema kuwa kupitia ushirikiano huo, hali ya usalama na matukio ya uhalifu yamepungua yakiwemo ya uhalifu, makosa ya usalama barabarani na kubwa zaidi wananchi wamesadiia kwa kiasi kikubwa kutoa taarifa zinazohusu masuala ya usalama.

"Nichukue fursa hii kuwashukuru wananchi wa Mkoa wa Iringa na niwaombeee waendelee na moyo huo huo wa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kwa pamoja tukomeshe vitendo vya uhalifu,"amesema.

Amesisitiza namna ambavyo jeshi la polisi limejipanga ili wananchi washerehe kwa amani na usalama na wale ambao wanakwenda kanisani waende bila wasiwasi.Pia wale ambao watakwenda kwenye kumbi za starehe nao waende bila hofu lakini kwa wale wenye kutumia vilevi na hasa pombe wasiliwe kupitiliza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...