Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), Suleiman Msuya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kufungua mafunzo ya kuwajengea waandishi wa habari kuandika habari za jinsia na usawa jijini Dar es Salaam leo.
Mkufunzi, Simbarashe Msasanuri, akitoa mada katika Semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika habari za jinsia na Usawa jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) jijini Dar es Salaam leo.
CHAMA cha wafanyakazi wa vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA) ndio chombo Sahihi kwa waandishi wa habari hasa wanawake ambacho kipo kwaajili ya kutetea haki zote mahala pakazi.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chama cha wafanyakazi wa vyombo vya habari (JOWUTA), Suleiman Msuya wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari hasa wanawake wa jijini Dar es Salaam kuandika habari za jinsia na usawa amesema kuwa waandishi wa habari wote wakiungana wanakuwa na sauti ya pamoja katika kutatua changamoto inapomkkabiri mwandishi wa habari ambaye atakuwa amejiunga na chama cha JOWUTA.
Msuya amesema kuwa Chama cha JOWUTA kimesajiliwa kwaajili ya kuwaunganisha waandishi wa habari na kuwa na lengo moja katika kuhabarisha umma.
"Waandishi wengi wakiwa katika vyombo vya habari hufanyiwa unyanyasaji, hawana mahala pa kusemea sasa JOWUTA ndio chombo sahihi kwaajili ya kutatua changamoto zinazowakumba waandishi wa habari wakiwa kwenye vyombo vyao".
Msuya amewaasa waandishi na wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika vyombo vya habari wajiunge na chama hicho kwani gharama za kujiunga ni ndogo ili kuwe na uwezekano wa kutetewa na chama litokeapo tatizo.
Kwa Upande wake Mwezeshaji wa masuala ya kijinsia, Simbarashe Msasanuri amesema kuwa ili kutatua changamoto za waandishi wa habari ni lazima waandishi wenyewe wavunje ukimya na kuandika vitendo vya unyanyasaji wowote unaotokea katika vyombo vyao.
Hata hivyo amesema kuwa pia mfumo dume katika vyombo vya habari lazima uondoke kwa waandishi wa habari wanawake kujituma na kuwania nafasi za uongozi zilizopo katika vyomo vya habari wanavyoviandikia.
Msasanuri amefafanua kuwa waandishi wa habarinwaachane na hali ya kuridhika pale walipo na waongeze juhudi ya kuweza kuendelea mbele.
"Muungane waandishi wa habari wanawake katika chama cha JOWUTA ili muwenze kuwa kitu kimoja na changamoto zitatatuliwa ".
Hata hivyo JOWUTA ni chama amacho kimesajiliwa mwaka jana na mpaka sasa kinawanachama 130, chama hicho ni chama cha wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika vyombo vya habari na sio waandishi tuu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...