Na Grace Gurisha
MENEJA wa Wakala wa Vipimo (WMA), Mkoa wa Kinondoni, Charles Mavunde amesema maeneo mengi ya Mkoa wa Dar es Salaam wamekuta matumizi ya mizani yapo sahihi ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
Mavunde amesema hayo leo, Desemba 9,2019 wakati alipofanya ukaguzi wa kushtukiza katika mabucha ya nyama yaliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujilidhisha kama vipimo vipo sahihi kwa mujibu wa sheria ya vipimo sura ya 340 , mapitio ya mwaka 2002 na kanuni zake.
Alisema wamepita kwenye mabucha mengi kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara na pia kila bucha wamebandika tangazo kuangalia vigezo muhimu ambavyo mtumiaji wa vipimo na mnunuzi anatakiwa kuvifuata.
Mavunde alisema kwa ujumla maeneo mengi waliyopita matumizi yapo sahihi na wafanyabiashara wanafuata sheria na wananchi wamehamasika na wamefahamu kwamba ni vitu gani ambavyo wanazingatia katika manunuzi ya nyama.
"Leo tumefanya ziara ya kushtukiza katika mabucha ya Mwenge kuangalia kama matumizi ya mizani yanafuata sheria za vipimo, kama tunavyofahamu kila baada ya miezi 12 inatakiwa kuhakikisha,
" Kwa ujumla tumekuta matumizi ya mizani yanafuata sheria za vipimo, tumekuta mabucha mawili yanatumia mizani miwili miwili ila mmoja ndiyo haujahakikiwa, watu hawa wamejaziwa fomu nakuchukuliwa hatua kadri sheria ya vipimo inavyoeleza,"alisema Mavunde
Kwa upande wake, Kaimu Meneja Mkoa wa Ilala, Saad Haruna alisema kama muuzaji wa atakuwa amesababisha kwa makusudi yeye mwenyewe kuutengua mzani ili usiweze kufanya kazi vizuri,atakuchukuliwa hatua za kisheria.
"Hatua za kisheria kwa wakala wa vipimo zipo za aina mbili faini au kwenda mahakamani na gauni inaanzia Sh.100,000 hadi Sh. Milioni 20. Kwa hawa watu wa mabucha adhabu yao inaanzia sh 100,000 hadi Sh 500,000," alisema.

Afisa
Vipimo namba Moja kutoka Wakala wa Vipimo nchini, Bw.Mohammed akitoa maelezo
kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu matumizi ya kifaa cha kupimia
vipimo vya kuuzia nyama, mara baada ya Kufanya ukaguzi wa Kustukiza katika mabucha
ya Mwenge Jijini Dar es Salaam mapema leo Desemba 09, 2019.

Mawakala wa Vipimo Tanzania wakiwa katika Bucha za Nyama maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukagua mizani kama ina viwango ambavyo vinatakiwa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...