NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
MBUNGE
wa Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, Mhe. Humoud Jumaa, ametoa rai kwa
Jumuiya ya Wanawake (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo
,kuanzisha miradi ili kujiimarisha kiuchumi na kuondokana na utegemezi.
Aidha
amewaasa waendelee kuwa na umoja kwenye jumuiya pamoja na kushirikiana
kuhakikisha chama kinashinda katika uchaguzi mkuu ujao wa madiwani,
wabunge na Rais.
Akizungumza
wakati anafungua baraza la mwaka la Jumuiya hiyo , mbele ya wabunge wa
Viti Maalumu Zaynabu Vulu na Hawa Mchafu, Jumaa alieleza, hatua hiyo
itasaidia kujiendeleza kimaendeleo wenyewe na kutatua mahitaji yao
madogo madogo badala ya kutegemea misaada.
"Nimefarijika
kuwa mgeni rasmi katika Baraza lenu la mwaka, niwapongeze kwa kazi
mliyoifanya wakati wa uchaguzi wa Wenyeviti wa Serikali za Vijijini na
Vitongoji, niwaombe m'buni miradi",
"Nina
marafiki wakubwa nitawaona pale penye mahitaji yatakayofaa kwenda
kuwaomba kunisaidia kwa ajili ya kuendeleza biashara zenu zitazokuwa
kitega uchumi kwa Jumuiya, huku nikishirikiana na wabunge wa Viti
Maalumu watawaunga mkono" alisema Jumaa.
Kwa
upande wake Mbunge wa Viti Maalumu Zaynabu Vullu ameendelea na ugawaji
wake wa vitendea kazi kwa Jumuiya mkoani hapa, ambapo alikabidhi boksi
tatu za karatasi kwa ajili ya shughuli za Jumuiya zilizoko ndani ya
Chama Cha Mapinduzi kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao.
Mwenyekiti
wa UWT wilayani humo, Leyla Humoud aliwashukuru wabunge wa Viti Maalumu
Zaynabu Vulu, Subira Mgalu na Hawa Mchafu, kwa namna wanavyoshirikiana
nao katika nyanja mbalimbali ili kuinua Jumuiya.
Leyla alitaka washikamane na kuwa wamoja kwani ndio nguzo pekee ya kusonga mbele.
wabunge wa
Viti Maalumu Mhe.Zaynabu Vulu na Hawa Mchafu wakipeana mkono
Mbunge wa
Viti Maalumu Mhe.Zaynabu Vullu akizungumza jambo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...