Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake ya mwisho kujiandaa na mchezo wa Shirikisho Azam Confederation Cup FA dhidi ya Iringa United hapo leo katika uwanja Uhuru jijini Dar es salaam, wakianza safari ya kutafuta nafasi ya kushiriki mashindano ya Kimataifa msimu ujao.

Katika mazoezi ya jana beki wa kulia Paul Godfrey 'Boxer' amerejea kikosini baada ya muda mrefu akitoka kuuguza majeraha ya muda mrefu.

Yanga msimu uliopita waliondolewa na Lipuli kwenye hatua ya nusu fainali ya baada ya kufungwa mabao 2-0.

Kaimu kocha mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya kushuka dimbani hapo leo na wanafahamu umuhimu wa mchezo huo na wanaiheshimu Iringa United hata kama inashiriki Daraja la Kwanza (FDL).

Mkwasa amesema, anafahamu bingwa wa mashindano haya anaiwakilisha nchi kwenye kombe la Shirikisho Barani Afrika na mnapocheza hakuna marudiano atakayeshinda anaenda hatua inayofuata, hivyo wamejipanga kuhakikisha wanapata matokeo.

Mbali na mchezo huo, Lipuli watakuwa wenyeji wakiikaribisha Dar City ya jijini Iringa uwanja wa Samora , Dar City inashiriki Ligi Daraja la Pili (SDL).

Kagera Sugar wao watakuwa Uwanja wwa nyumbani wa Kaitaba kuikaribisha Rufiji United inayoshiriki ligi daraja la pili ambapo kocha wa timu hiyo, Mecky Mexime amesema wanauchukulia mchezo huo kwa umuhimu mkubwa kwani lengo lao ni kusonga kushinda na mbele zaidi.

Kikosi cha Yanga kikiwa mazoezi leo Katika Uwanja wa Uhuru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...