Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

IMEELEZWA kuwa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Karibu Tanzania Organization (KTO) imekuwa ni moja kati ya washiriki bora katika kuisaidia Serikali katika kutatua changamoto za kijamii hasa katika masuala ya elimu, ujinsia na kusaidia watoto wa kike katika kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukatili wa kijinsia.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufungaji wa mafunzo maalumu ya siku tano kwa walimu na wakufunzi kutoka vyuo maendeleo ya  wana nchini nchini Katibu Mkuu kutoka Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamiii Dkt. John Jingu amesema, KTO ni moja kati ya wadau muhimu ambao wamekuwa waliofanya kazi na Serikali kwa ukaribu zaidi.

"Nianze kwa kutoa pongezi kwa taasisi hii hasa kwa kuendelea kumlinda na kumwendeleza mtoto wa kike Tanzania, mmekua mkishirikiana na Serikali katika kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi na
Programu hii iliyowakutanisha ya kozi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali kwa watoto chini ya umri wa miaka 5 kupitia vyuo vya maendeleo ya wananchi ni muhimu na kubwa zaidi mmeangalia masuala ya kijinsia na malezi:  tunahaidi kuendelea kutoa ushirikiano ili tuweze kufikia azma tuliyojiwekea hasa katika kumwezesha mtoto wa kike" ameeleza Dkt. Jingu.

Amesema kuwa Asasi za kiraia zifanye kazi kwa ukaribu na Serikali katika kushughulikia matatizo ya wananchi na kueleza kuwa kupitia programu hiyo ya malezi na makuzi kwa watoto ni muhimu sana  kwa kuwa msingi mkuu  wa malezi kwa mtoto ni katika miaka  5 tangu kuzaliwa ambayo ndio muhimu katika misingi ya ukuaji kwa watoto kiakili, kimaono na kihisia.

"Watoto ndio msingi wa taifa, jinsi watoto wanavyolelewa sasa ndio picha ya taifa la kesho litakavyokuwa na tuna mpango wa kuwa na vituo vya malezi nchi nzima kwa malengo ya kuwajenga ili wawe wazalendo, wachapakazi pamoja na kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili vinavyofanywa hata na wanafamilia lakini pia vituo hivyo vitawasaidia watoto kutoa taarifa na watakuwa salama zaidi" Ameeleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa elimu ya mafunzo ya ufundi (TVET) Dkt. Noel Mbonde amesema kuwa KTO ni wadau wakubwa katika sekta ya elimu na programu za taasisi hiyo pia zimeisaidia pia Wizara hiyo katika kuboresha utoaji wa huduma bora zaidi.

" Ninaamini kwamba Wizara imepata mwarobaini wa changamoto za watoto wa kike kuacha shule kwa matataizo mbalimbali ikiwemo mimba za utotoni, tutawapeleka kwenye vyuo hivi ili wapate elimu  na watoto wapate malezi bora" ameeleza.

Amesema kuwa takribani shilingi bilioni 38 zimetengwa katika kuhakikisha kila Chuo cha maendeleo ya jamii kinakuwa na darasa la chekechea ambapo hadi sasa madarsa 20 yamekamilika, 20 yanajengwa na hadi kufikia Aprili 2020 vyuo vyote vitakuwa na madarasa hayo.


Awali akitoa maelezo kuhusiana na taasisi hiyo Mkurugenzi wa miradi (KTO) Mia Mjengwa amesema kwa siku hizo tano wametoa mafunzo kwa vitendo ambayo wanaamini yataleta tija katika sekta ya elimu na kueleza kuwa ni muhimu sana kuwa na vituo vingi vya chekechea kutokana na misingi ya malezi na makuzi ya watoto huanzia hapo.

Amesema kuwa wakufunzi  kutoka vyuo vya maendeleo  ya wananchi wana nafasi kubwa sana katika kuleta maendeleo kwa kuwa wanafanya kazi kwa ukaribu zaidi na wanajamii.

"Miaka ya 60 Hadi 70 Sweden ilianza kuwa na elimu ya chekechea naamini ni sawa na hapa Tanzania, na kwa sasa taifa limejiegemeza katika kujenga uchumi, Hapa Kazi Tuu! kadri maendeleo yanavyokua akina mama wanajishughulisha katika shughuli za maendeleo hivyo lazima kuwe na sehemu sahihi na salama za kuwaacha watoto wetu" ameeleza.


Pia mwenyekiti wa Bodi ya KTO Aidan mchawa amesema kuwa
Serikali imeendelea kushirikiana na taasisi hiyo kupitia  Wizara za afya na elimu ambao wamekuwa wakishirikiana katika kufanikisha programu hiyo;

"Wizara ya elimu, kupitia idara ya elimu  imeonesha ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha KTO inasonga mbele zaidi, na tanaamini tutafika mbali na tunaomba Wizara kushirikiana nasi katika kuendesha mafunzo ya namna hii kwa vyuo vyote 54 vilivyopo nchini" ameeleza.

Baadhi ya washiriki ambao ni wakufunzi waliohudhuria kikao kazi hicho wameonesha kufurahishwa kwa namna serikali inavyoshirikiana na asasi za kiraia katika kutatua changamoto za kijamii.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamiii Dkt.John Jingu akizungumza wakati wa kufunga mafunzo maalumu ya siku tano kwa walimu na wakufunzi kutoka vyuo vya maendeleo ya wananchi nchini ambapo  amesema kuwa Serikali kupitia Wizara hiyo wataendelea kushirikiana na taasisi hiyo katika kutatua changamoto za wananchi, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Karibu Tanzania Organization (KTO) Maggid Mjengwa akizungumza wakati hafla ya  ufungaji wa mafunzo hayo na kuwataka wawezeshwaji kutumia maarifa waliyoyapata katika kuleta matokeo chanya katika jamii, leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa miradi (KTO) Mia Mjengwa akitoa taarifa ya kikao kazi hicho kilichofanyika kwa siku tano na kueleza kuwa malezi wapatayo watoto sasa ni picha ya taifa la baadaye hivyo lazima wapate elimu Bora ya makuzi, uadilifu na kufanya kazi. Leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa elimu ya mafunzo ya ufundi (TVET) kutoka Wizara ya Elimu Dkt. Noel Mbonde akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo ambapo amesema kuwa vyuo 54 vya maendeleo ya wananchi lazima viwe na madarasa ya chekechea na mchakato umeanza na utakamilika Aprili 2020 kwa bajeti ya shilingi bilioni 38, leo jijini Dar es Salaam
Mkufunzi wa Chuo Cha maendeleo ya  Wananchi Felister Nanguka akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo hayo ambapo ameishukuru Serikali kupitia Wizara kwa kushirikiana KTO katika kuleta maendeleo kwa jamii, leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...