Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
SUALA
la baadhi ya mitandao ya simu nchini kufunga laini kabla ya tarehe
elekezi ya kufunga laini hizo ambayo ni Desemba 31 mwaka huu.
Waziri
mwenye dhamana ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack
Kamwelwe amesema kuwa kufikia Desemba 31 laini zote za simu ambazo
hazijasajiliwa kwa alama za vidole na namba za kitambulisho cha uraia
zinazotolewa na (NIDA) zitakatwa na kile kinachoelezwa kuwa baadhi ya
mitandao imeanza kufunga laini hizo ni kukumbushwa kuwa watazikata laini
zote zisizo na usajili.
Akijibu hoja ya kwanini baadhi ya makampuni ya simu yamefunga laini za simu kabla ya wakati Mhandisi Kamwelwe amesema;
"Zoezi
la usajili litakamilika tarehe 31 Desemba mwaka huu, na tutakata laini
zote zisizosajiliwa kwa kutumia namba za NIDA na alama za vidole"
amesema.
Aidha amesema
kuwa watanzania wengi wamekuwa wakiibiwa kutokana na umiliki holela wa
laini za simu ambapo mtu mmoja anaweza kumiliki laini za simu zaidi ya
mia moja.
"Kenge hasikii
hadi damu itoke puani, mlikuwa mnashtuliwa tutakata laini zote zisizo na
usajili kufikia Desemba 31 mwaka huu" amesema.
Hayo
ameyasema leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kushuhudia utiwaji
saini wa makubaliano ya ujenzi wa jengo la makao makuu ya umoja wa
shirika la Posta Barani Afrika, Pan African Postal Union (PAPU) umoja
ulio na nchi wanachama 45 na jengo hilo litajengwa jijini Arusha
Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...