Na Grace Gurisha

TAASISI ya Mabolozi wa Usalama Barabarani Tanzania ( RSA), imewataka madereva kwa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kuwa makini kwa kuendesha ule udereva unaotakiwa wa kujihami.

Hayo yalisema mwishoni mwa wiki na Balozi wa Usalama Barabarani, Augustus Fungo wakati walipotembelea kituo cha mabasi ubungo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuendeleza kampeni ya panza sauti kwa kutoa elimu kwa madereva na abiria sambamba na ukaguzi wa mabasi.

Pia, Fungo alisema kuwa wametembelewa na Muungano wa Jumuiya za Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kutoka Pemba, ambao wamekuja kujifunza kutoka kwao jinsi ambavyo wanafanya kazi, ambapo na wao walitoa elimu katika kituo hicho.

Fungo alisema kwa nini wanafanya mwisho wa mwaka, ni kwa sababu wanaongeza mkazo kutokana na kwamba kipindi hicho kinakuwa na abiria wengi wanaosafiri na pia ni kipindi ambacho watu wanaingia na magari barabarani kwa mara ya kwanza.

"Katika kufanya hivyo hata yule dereva mwingine mzembe aliyekuwepo barabarani unaweza kumkwepa na kuokoa maisha yako na ya wengine ambao umewapakia katika hilo gari, kwa hiyo udereva wa kujihami unahitajika," alisema Fungo.Alisema ajali za barabarani ni janga kubwa duniani kote, ambapo watu milioni moja laki tatu na nusu wanafariki kila mwaka.

"Hii ni sawa na kusema katika kila sekunde 24 kuna mtu mmoja anafariki kwa ajali za barabarani. Hapa kwetu Tanzania ajali zimepungua kwa mwaka huu hadi kufika Agosti tumekuwa na ajali 1096,lengo ni kuhakikisha ajali zinakuwa chini,"

"Hatuangalii sana ajali tunaangalia kwamba hata kama ajali zitatokea basi yale madhara vifo pamoja na majeruhi yaweze kupungua sana, kwa sababu haya ndiyo yanaleta mzigo wa taifa , " alisema Fungo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mdhibiti wa Latra, Johansen Katano alisema RSA wanafanya kazi kubwa ya kuwahamasisha abiria na madereva wa magari ili kuzingatia sheria za u salama barabarani.

"Hivi sasa watu wameanza kuelewa wajubu wao, awe ni abiria, dereva au wamiliki, kwa hiyo ukiona mabadiliko ujue ni kazi kubwa imefanywa.

Pia, Mkurugenzi huyo akitoa onyo kwa wamiliki wa mabasi, madereva na wafanyakazi wao has a mawakala kupandisha nauli kiholela kwa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka na pia amewaonya wamiliki watakaoingiza magari mabovu barabarani.

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Mabasi Tanzania (Wamata), Majura Kafumu alisema wanapamba sana na suala la usalama barabarani kwa kushirikiana na jamii zingine na abiria wenyewe.

" Kungekuwa na mfumo mmoja wa kuajili na mamlaka moja, hii itasaidia kuajili madereva wenye sifa na ajali zingeendelea kupungua, kwa sababu kuna Kampuni zingine wanapenda madereva wa kipacho cha chini ambao ndiyo wanaowasababishia mambo mengi kutokea,"alisema Kafumu




Ukaguzi wa mabasi mbali mbali ya ubiria yakifayiwa ukaguzi kabla ya kuanza kwa safari katika kituo cha Mabasi cha Ubungo,jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...