Meli ya MV. Nyakibalya ikiwa katika Bandari ya Bukoba mkoani Kagera.Meli hiyo ni maalumu kwa ajili ya kubeba mizigo ndani ya Ziwa Victoria.
Meneja
wa Bandari za Kanda ya Ziwa Morris Mchindiuza akizugumzia hatua
mbalimbali za uboreshaji wa miundombinu katika Bandari ya Bukoba mkoani
Kagera.
Ofisa
wa Bandari ya Bukoba iliyopo mkoani Kagera Bulenga Komagi akizungumza
na waandish wa habari kuhusu umuhimu wa bandari hiyo kwa wananchi wa
mkoa huo na nchi jirani.
Jengo
la utawala katika Bandari ya Bukoba mkoani Kagera likiwa limefanyiwa
maboresho.Jengo hilo lilijengwa mwaka 1945 ambalo lilikuwa linatumiwa
tangu enzi za ukoloni.
Na
Said Mwishehe, Michuzi Globu -Bukoba
BANDARI
ya Bukoba mkoani Kagera imetejwa kuwa miongoni mwa bandari sita kubwa zilizopo
katika Ziwa Victoria ambazo zipo chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania(TPA.
Kwa mujibu wa TPA, bandari hiyo ndio chachu ya wafanyabiashara wa Mkoa wote wa Kagera
hususani Bukoba Mjini ambao hudumia
bandari kwa ajili ya kusafirisha shehena ya mizigo ya mazao ya kilimo pamoja na bidhaa mbalimbali kwa ajili
ya mahitaji ya wananchi.
Akizungumza leo
Desemba 12, mwaka 2019, Meneja wa Bandari za Kanda ya Ziwa Morris Mchindiuza
amefafanua bandari hiyo ilijengwa mwaka
1945 enzi za mkoloni na baada ya uhuru ikawa chini ya Shirika la Reli na
Bandari ya Afrika Mashariki mpaka ilipofika mwaka 1977 baada ya
Jumuiya
ya Afrika Mashariki kuvunja ikwa chini ya Shirika la Reli Tanzania(TRC).
"Ilipofika
mwaka 1997 ikawa chini ya Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania( MSCL) ambao
kampuni hiyo waliendelea kuihudumia bandari mpaka mwaka 2004 ilipoundwa Sheria
ya TPA kwa Sheria namba 17 ikawa chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari
Tanzania.
"Bandari
hii ni kongwe na ilikuwa na miundombinu iliyokuwa imechakaa na hivyo TPA
tukaamua kuiboresha miundombinu yake.Tunatarajia baada ya kukamilika bandari
hii itarejea tena katika shughuli zake hasa kwa kutambua kuanzia mwakani meli
ya MV Victoria inatarajiwa kuanza tena safari zake,"amesema.
Ameongeza
mradi wa kuboresha bandari hiyo pamoja na maeneo mengine umegusa pia majengo ya
abiria ambapo kulikuwa na uboreshaji wa
awamu mbili, ya kwanza ilishakamilika na awamu ya pili imekamilika hivi
karibuni.
"Katika
maboresho haya tumetumia gharama ya shilingi milioni 565 kwa kazi hii ya kuhuisha jengo
zima la abiria na jengo la utawala, kwa sasa hivi kila kitu kimekamilika na kwa
upande wa huu.
"Pia
tunaendelea na ukarabati wa majengo ya kuhifadhia mizigo ambao nao huu upo
katika mradi mwingine wa uboreshaji a miundombinu ya Bandari kwa eneo la
Bukoba, Kemondo, Mwanza Kaskazini na Kusini,"amesema Mchindiuza.
Ameogeza
miaka ya nyuma kidogo kulikuwa na meli za MSCL ambazo zilifanyakazi ikiwamo
meli ya Mv. Bukoba iliyoanzia katika bandari hiyo hadi bandari ya Mwanza, Meli ya Mv. Victoria nayo ilikuwa
ikija hapa pamoja na meli ya na Mv Serengeti.
"Tunatarajia
meli ya Mv.Victoria kuanzia mwezi wa mwakani itarudi kwenye safari zake na
kubeba shehena.Kwa kipindi hiki tumekuwa tukiendelea kutoka huduma hasa kwa wateja
wakubwa wawili ambao ni Kagera Sugar ambaye amekuwa akitumia bandari hii
kusafirisha sukari kutoka hapa kwenda Mwanza.
"Mteja
mwingine tunayemuhudumia ni mfanyabiashara Omukwano ambaye yeye amekuwa akileta
bidhaa za madukani kama mafuta, sabuni kutoka nchini Uganda mpaka hapa Bukoba
kwa ajili ya soko la hapa kwetu,"amesema.
Kuhusu
uwezo wa bandari hiyo ameeleza imekuwa ikihudumia tani 6000 pamoja upande la
jengo la abiria linauwezo wa kuwa na abiria 400 kwa wakati mmoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...