Na.Khadija seif, Michuzi TV

KAMPUNI ya Kitanzania inayolenga kukuza utalii wa ndani (Wonderland) Imezinduwa rasmi Tamasha jipya liitwalo Masaai Festival, ambalo linatarajia kufanyika mwanzoni wa mwaka 2020 Texas Marekani.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Said Maulid amesema wameandaa tamasha la maasai kwa lengo la kutoa mchango mkubwa kwenye swala la zima la utalii na pia juu ya maendeleo ndani ya sekta hiyo ya utalii.

“Wonderful imeandaa ili tamasha kwa lengo la kukuza utalii na kutangaza utalii nje na ndani ya Tanzania,"Pia Maulid ametambulisha mabalozi ambao wataenda kushiriakiana nao kwa lengo la kulitangaza tamasha pamoja na kuhamasisha watanzania kuwa wazalendo kupenda vitu vya kinyumbani zaidi.

Ndani ya mabalozi hao wapo wasanii wa mziki kama G nako kutoka kundi la weusi, Mrisho Mpoto (mjomba), mwigizaji batuli, Welu sengo na wengine wengi.Moja kati ya mabalozi waliopata nafasi ya kuzungumza ni Batul ambae ni muigizaji wa filamu.

"Hiki ni kitu kikubwa na tumeungana kama watanzania kutangaza utalii wetu na tunategemea tutapata muitikio mzuri kwani ni ” tamasha la kipekee ambalo litavuka hadi nje ya nchi kwa lengo la kujitangaza kitalii zaidi,"

Hata hivyo batul ameeleza sababu za kuchaguliwa kwa wa masai Ni kutokana na kabila Hilo kudumu kwenye tamaduni zao kwa muda mrefu kuanzia mavazi,vyakula na rafudhi zao kuwa kama kielelezo tosha.

"Wamasai ni Kama kielelezo tu ila tunategemea kuwepo na Makabila mengi zaidi na kuhamasika kupitia sekta hiyo ya utalii na kupelekea kuongeza pato la taifa,"
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Wonderland Said Maulid akisikiliza swali kutoka kwa mwandishi wa habari huku akiwa na mabalozi Batuli,well sengo,g nako pamoja na Mrisho mpoto
Mkurugenzi wa Kampuni ya Wonderland Said Maulid akizungumza na waandishi wahabari kuhusu tamasha la Masai linalotarajiwa kuanza mwakani huku akiwa na balozi wa tamasha Hilo là kitalii Batuli muigizaji wa filamu nchini.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...