Na.Catherine Sungura, Dodoma.
Jumla ya sampuli 5106 zimefanyiwa uchunguzi katika maabara zikiwemo za masuala ya kijamii na kijinai katika mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali kanda ya kati.

Hayo yamesemwa na Meneja wa mamlaka hiyo kanda ya kati Musa Kuzumila wakati wa ziara ya maofisa habari wa wizara ya afya na taasisi zake wakati wa kutembelea mamlaka hiyo kujionea mafanikio yaliyofanywa katika kuboresha sekta ya afya nchini.

Kazumila amesema kwamba tangu kuanzishwa kwa kanda hiyo miaka miwili na nusu sasa ,kanda yake imefanikiwa kupima sampuli hizo ambazo zimefanyiwa uchunguzi katika maabara na kuzitolea ushahidi mahakamani

"Mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu inasimamia sheria na kudhibiti kemikali hivyo tumeweza kufanyia uchunguzi sampuli na hivyo kupunguzia wateja umbali na hivyo kusaidia wananchi kupata haki na kutoa ushahidi kwa wakati".Amesema Kazumila.

Kwa upande wa vinasaba Kazumila amesema kati ya sampuli walizopokea jumla ya sampuli 36 zilizowasilishwa asilimia 90 zilikua zinaangalia uhalali wa baba wa mtoto.

Hata hivyo amesema kwamba mamlaka hiyo imeweza kukagua maeneo yanayojihusisha na kemikali zipatazo 360 pamoj na kutoa vibali 139 za kuingiza na kusafirisha kemikali nchini kwa kanda ya kati.

Kwa upande wa wajasiriamali wadogo wadogo mamlaka hiyo imewapatia mafunzo wajasiriamali 315 namna ya matumizi salama ya kemikali pamoja na kutoa elimu kwa wachenjuaji wa dhahabu wanaotumia kemikali aina ya sodium cyanide.

Mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali kanda ya kati inahudumia mikoa ya morogoro,iringa,dodoma,singida na tabora na ilianzishwa mwaka 2017.
Meneja wa kanda ya kati ya mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali Musa Kazumila wakati akiongea na maofisa habari wa wizara na taasisi zake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...