Shindano la kuibua vipaji kwa wanafunzi wa shule za msingi jijini Dodoma nchini Tanzania limehitimishwa jana Jumatano Desemba 4, 2019 kwa shule ya msingi Chadulu kuibuka mshindi wa Jumla na kunyakua kitita cha TSh500,000.

Shindalo hilo lililojulikana kama Mavunde Talent Search 2019 lilianza Novemba 25, 2019 kwa kushirikisha shule 25 zilizokuwa na washiriki 500 kwa ufadhili wa mbunge wa Dodoma Mjini (CCM),  Mh Anthony Mavunde.

Lengo la shindano hilo lilikuwa kuibua vipaji katika mpira wa pete, miguu, uimbaji, kompyuta na uchoraji ambapo wanafunzi walionyesha uwezo mkubwa hasa katika uimbaji.

Shule zilizoibuka na ushindi wa jumla ni Chadulu ikifuatiwa na DCT Bishop Stanley na ushindi wa tatu ulikwenda kwa shule ya msingi Mlimwa.

Akitoa zawadi kwa washindi bora 20, mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini, Mh Patrobasi Katambi amesema shindano hilo linatoa nafasi nzuri kwa washindi ambao sasa watakwenda kusomeshwa katika Shule ya Ellen White English Medium  ambayo inakuza vipaji.

"Mbunge wenu amewalipia ada katika shule hiyo na ametoa vifaa vyote muhimu ambavyo vinatakiwa kwa wanafunzi, mbali na zawadi za shule lakini watoto watasimamiwa kikamilifu kwenye taaluma," amesema Katambi.

Aidha,Wazazi wa wanafunzi hao 20 ambao watapata ufadhili wa masomo ya kawaida na mafunzo ya kuendeleza vipaji vyao katika *Shule ya Ellen White English Medium * wamemshukuru Mbunge Mavunde kwa jitihada kubwa anayoifanya kwenye kukuza elimu na vipaji katika Jimbo la Dodoma Mjini.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patribasi Katambi akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Ellen White English Medium wakati wa utoaji wa zawadi kwa shule zilizifanya vizuri katika Shindano lililoandaliwa na Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde.
 Mwanafunzi akionesha umahiri wa kutumia vifaa vya muziki.
 Mkuu wa Wilaya wa Dodoma Patribasi Katambi akizungumza na wazazi na Wanafunzi wa Shule ya Ellen White English Medium katika utoaji zawadi kwa wanafunzi wenye vipaji lililoandaliwa na Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...