Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
RAIS
wa zamani wa Pakistan, Pervez Musharraf (76) amehukumiwa kifo katika
kesi ya Uhaini mkubwa iliyohusisha kuweko kwa dharura ya Kikatiba nchini
humo mnamo mwaka 2007.
Wakati
wa hali ya dharura, Mahakama kuu haikupitisha hili hivyo Pervez
aliamrisha kukamatwa na kuteswa kwa wanasiasa na mawakili ambao walikuwa
kinyume na yeye.
Jumanne
ya Desemba 17, amehukumiwa kwa mashtaka hayo katika mahakama kuu mjini
Islamabad na kuweka historia nchini humo kwa kuwa kiongozi wa kwanza wa
kijeshi kuhukumiwa akiwa madarakani.
Baada
ya kuondolewa madarakani na jeshi hilo mwaka 1999, hadi sasa jeshi la
nchi hiyo linaendelea kudhibiti masuala ya usalama, ulinzi pamoja na
sera za ndani na nje ya nchi.
Aidha
Chama cha uislamu cha Musharraf's All Pakistan Muslimu League (APML)
kimeeleza kuwa watakata rufaa mapema, huku ikinukuliwa kuwa kuwa
Musharraf alienda nchi za kiarabu 2016 na kukataa kuhudhuria na
kujitetea juu ya kesi iliyokuwa inamkabili na aliondoka nchini humo na
kwenda Dubai kwa matibabu na video iliyochukuliwa kutoka hospitali hapo
imeonesha kuwa aliruhusiwa mapema mwezi huu.
Hadi
hukumu hiyo inatolewa kiongozi huyo akiwa Mjini Dubai tangu alipoondoka
Machi 2016 kwasababu za Kiafya. Musharraf alitolewa madarakani mwaka
1999 kwa mapinduzi ya kijeshi.
Tusisahau, Bado anahusishwa na Mauaji ya Benazir Bhutto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...