Baada ya kimya cha muda mrefu, Mzungu Kichaa amerudi
na singo mpya. You Got Me ni
wimbo ya mapenzi inayogusia hitaji la kupendwa kwa kila mwanadamu.
Mashairi na upigaji stadi wa gitaa na bass kutoka kwa
Mzungu kichaa vimebeba wimbo. You Got Me ni nyimbo ya kwanza kutoka kwenye
album mpya ya Mzungu Kichaa inayoitwa “Huyu nani” itakayotoka mapema mwaka
2020.
We don’t have time (hatuna muda) / To take it slow (kuwa watulivu) / Cos the future (sababu kesho yetu) / We will never know (hatuijui)
Be open (uwe muwazi) / Be free (uwe huru) / Take
a chance (itumie nafasi hii) /Jump on to the other side with me (ruka upande wa
pili pamoja nami)
Khalid Kumbuka aka KK, ni kaka mdogo
wa Adili mmoja wa waasisi wa kundi la kwanza la Hipihop Tanzania Kwanza Unit,
ambaye alifariki katika ajali mbaya ya gari Dar es salaam mwaka 1992. Mzungu
kichaa alipokuja Tanzania katikati ya miaka ya 90 mama yao Margarethe Kumbuka
ndiye alimfundisha Kiswahili katika shule ya sekondari Dar es Salaam. Baada ya
kuhamia London kusoma Chuo kikuu na mama Margarethe alihamishiwa chuo hicho
hicho kufundisha Kiswahili na wote wakafanya masters pamoja. Baadae Mzungu
kichaa alipogundua kipaji cha Khalid Kumbuka kwenye uandishi na kutumbuiza,
ilikuwa rahisi kumualika studio na kufanya kazi pamoja.
Magitaa mawili yamechanganywa kwenye
kiitikio na kutoa hisia ya kipee kutokana na upigaji wa gitaa wa Mzungu kichaa.
Aina ya sauti ambayo amekuwa akiitengeneza tangu siku za awali kwenye Bongo
Flava ambapo mtiririko wake wa gitaa ulisikika kwenye She Gatta Gwan wa
Mangwaire na Mambo ya Pwani ya Solo Thang. Kwenye You Got Me, P Funk Majani alimjaribu
Mzungu Kichaa kupiga gitaa la Bass na kuongezea ubunifu wake kwenye kuzalisha
maadhi ya Trap hi-hat na kiki nzuri na snare. Pasipo shaka hii ni kazi bora
iliyotokana na uzoefu wa muda mrefu.
CREDITS
Track: You Got
Me
Featuring:
KK, Grace Matata
Produced by:
Mzungu Kichaa and P Funk Majani
Recorded at:
Caravan Records and Bongo Records
Mixed by:
P Funk Majani
Mastered by:
Jacob Brondlund
Record Label:
Caravan Records
Video Director:
Jessica Maria Olsen
Video Editor:
Carlo Kamin
Video Grading: Justin
Campo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...