Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni alipowasili katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania tayari kwa hafla ya ufungaji Mafunzo ya Uongozi ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza leo Desemba 17, 2019 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni akikagua Gwaride lililoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza lililofanyika Desemba 17, 2019 katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni akiwa katika jukwaa kuu tayari kwa kupokea salaam ya heshima kutoka Gwaride lililoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza lililofanyika Desemba 17, 2019 katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni (kushoto) akimvisha cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Magereza mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza ambaye amefanya vizuri zaidi katika Mafunzo hayo.
Kundi la Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi ngazi ya juu wa Magereza wakipita mbele ya Mgeni rasmi katika Sherehe za kufunga Mafunzo ya Uongozi ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza lililofanyika Desemba, 2019 katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa toka Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Wageni waalikwa meza kuu wakifuatilia Gwaride la wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza kama wanavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwa Wahitimu.
Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi kama wanavyoonekana katika picha.
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Joel Matani akiwa na Maafisa Waandamizi kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakifuatilia Sherehe za ufungaji mafunzo hayo ya Uongozi ngazi ya juu, leo Desemba 17, 2019(Picha zote na Jeshi la Magereza).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...