Charles James, Michuzi TV

MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioisha mwezi Novemba mwaka huu umeongezeka hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioisha mwezi Oktoba.

Hiyo inamaanisha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2019 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuepo kwa mwaka ulioisha mwezi uliopita.

Akizungumza na wandishi wa habari leo, Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ruth Minja ambapo amesema ongezeko la mfumuko wa bei limesababishwa na mahitaji makubwa ya bidhaa pamoja na usafirishaji.

Amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioisha kumechangiwa na ongezeko la bei za bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoisha Novemba mwaka huu zikilinganishwa na bei za mwezi Novemba mwaka jana.

" Bidhaa za vyakula zilizoongezeka bei kwa mwezi huu kulinganisha na mwaka jana ni pamoja na Mchele kwa asilimia 6.6, Unga wa Muhogo asilimia 7.8, Nyama asilimia 2.6, Mafuta ya Kupikia asilimia 7.2, Maharage asilimia 8.6, Mbogamboga asilimia 6.0 na Mihogo kwa asilimia 5.8," Amesema Minja.

Amesema kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula zilizoongezeka bei kwa mwezi huu kulinganisha na Novemba 2018 ni pamoja na mavazi asilimia 2.7, Mkaa asilimia 4.4, Samani asilimia 3.1, Huduma ya Malazi kwenye nyumba za wageni asilimia 5.0 na mazulia kwa asilimia 6.3.

Pia mfumuko wa bei za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2019 umeongezeka hadi asilimia 6.1 kutoka asilimia 5.1 kwa mwaka ulioisha Oktoba 2019.

Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Bi Ruth Minja akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...