

***********************************
Benki Kuu ya Tanzania
ikishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama imeendesha operesheni ya
kukamata watengenezaji na wasambazaji wa noti bandia nchini.
Operesheni hio iliyofanyika
katika Mkoa wa Kilimanjaro na Dar es Salaam, ilifanikisha kukamatwa kwa
watuhumiwa wawili ambapo mmoja wao ni wakala mkubwa mjini Moshi mkoani
Kilimanjaro na mwingine ni mkazi wa Chanika ambaye ni mtengenezaji na
msambazaji wa noti bandia jijini Dar es Salaam.
Katika upekuzi uliofanywa na
kikosi kazi kilichosimamiwa na jeshi la polisi, fedha bandia pamoja na
mitambo mbalimbali na vifaa vyakutengenezea noti hizo vilipatikana
ambavyo ni pamoja na
- Scanner
- Vibao vyenye vichwa vya picha za marais mbalimbali walioko kwenye noti za kila nchi
- Wino na rangi za aina mbalimbali zinatotumika kutengeneza noti bandia
- Brush za kusafishia wino uliopakwa kwenye karatasi
- Mashine ya kugandisha wino kwenye karatasi (lamination machine)
- Desktop Computer aina ya dell na monitor aina ya HP ambayo hutumika kuchanganya rangi za noti kwakutumia software ya Adobe
- Colored printer aina ya Xerox wanayotumia kuchapisha noti bandia
- Mashine yakubana foil paper kwenye noti bandia ili kuipa mng’ao kama noti halisi
- Mashine ya kukatia karatasi zenye picha ya noti ili ziwe katika sura
Vielelezo vilivyokamatwa ni
- Noti za 10,540 Tanzania zenye thamani ya Tshs 11,748,000.00 (kama zingekua halali)
- Noti 133, 048 za Marekani zenye thamani ya dola 13,302,400 (kama zingekua halali)
- Noti 11,0233 za Mozambique zenye thamani ya Tshs 290,464,259.98 (kama zingekua halali)
- Noti 2270 za Kwacha ya Demokrasia ya Kongo zenye thamani ya KWACHA 4,302,000 (kama zingekua halali)
- Noti 1 ya shilingi ya Kenya yenye thamani ya Kshs 200
- Noti 1 ya Kwacha 500 za Malawi
Karatasi 65 zenye picha za pesa
za nchi mbalimbali kama vile Malawi, Zambia, Dola za Marekani, DRC
Congo, Tanzania, Botswana na Mozambique
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...