Na Leandra Gabriel, Globu ya Jamii.

Ni ajabu na nadra  kutokea katika jamii ya sasa kuona wanyama au ndege wakipata nafasi ya kutambulika kutokana na muonekano wa kuvavuta wengi, Lil Bub ambaye ni paka aliyevunja rekodi ya kuwa  mashuhiri hasa katika mtandao wa Instagram ambako amekuwa akifuatiliwa na wafuasi zaidi ya milioni mbili, Lil Bub amefariki akiwa na umri wa miaka nane, mmiliki wa Paka huyo Mike Bridavsky amethibitisha kupitia ukurasa wa Instagram wa Paka huyo na kueleza kuwa Lil alifariki akiwa usingizini.

Lil Bul ambaye aliwavuta wengi kwa muonekano wake wa kuwa na ulimi mdogo, picha zake pamoja na kutokuongezeka kimo jambo lililomfanya aendelee kuwa na muonekano mdogo na hiyo ilimfanya kuwa paka pekee kugundulika kuwa na tatizo hilo la homoni (dwarfism)

Wengi wamemwelezea Lil kuwa ni mtunzi, mtangazaji wa Televisheni na msemaji wa wanyama ulimwenguni.

Kupitia Lil Bub dola za kimarekani zipatazo 700,000 zilipatikana ili kuwasaidia wanyama wenye mahitaji maalumu kama yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...