Mamia ya wananchi wa mkoa wa Morogoro na Wilaya zake, wanachama na wakereketwa wa CCM, wanachama wa vyama mbali vya siasa, viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali wakiongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo 24 Disemba 2019 wamehudhuria na kushiriki mazishi ya *Mama mzazi wa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Innocent Kalogeris
Mama Theodora Vasos Kalogeris amefariki dunia Jumapili 22 Disemba 2019 Hospital ya Chuo cha Kilimo (SUA) Morogoro na kuzikwa leo alasiri makaburi ya Kola Hill Morogoro Mjini.
Mapema viongozi na wanachama walipata kuaga mwili kisha kufanyiwa ibada fupi nyumbani kwake Mji mpya na baadae kufuatiwa na Ibada ya mazishi kanisa la Kuu St Patrick.
Viongozi wengine walishiriki Mazishi hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Katibu Mkuu wa UWT, Wabunge kutoka mkoa wa Morogoro na Mbunge wa jimbo la Korogwe Marry Chatanda, Wakuu wa Wilaya zote za mkoa huo, IGP mstaafu Mahita, Mwenyeviti wa Chama wa Wilaya zote wakiongoza kamati za siasa za Wilaya zao, wakuu wa vyombo vya ulinzi na ulinzi na Usalama mkoa huo, wakuu wa taasisi za umma pamoja na ndugu jamaa na marafiki.
Mwendo Umeutimiza, Pumzika kwa Amani
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza jambo na Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro , Shaka Hamdu Shaka na pichani kati ni MKuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loatha Sanare wakati wa mazishi ya Mama mzazi wa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Innocent Kalogeris
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...