Wamiliki wa viwanda mkoa wa Waziri wa
Nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji,Mhe Angela Kairuki wakati akifanya ziara ya
kutembelea viwanda mkoani morogoro orogoro walalmikia sheria ya
ushuru wa forodha ya East Africa sambamba na VAT kukwamisha ukuaji wa
viwanda vya ndani hali inayo fanya
washindwe kushindana na viwanda vya nje ya nchi.
Wamiliki hao wameeleza changamoto hizo mbele ya Waziri wa
Nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji,Mhe Angela Kairuki wakati akifanya ziara ya
kutembelea viwanda mkoani Morogoro na kujua changamoto zao sambamba na namna
gani ya kutatua.
Aidha badhi ya changamoto zilizo lalamikiwa ni pamoja na
sheria ya ushuru ya Afrika Mashariki zinazo daiwa kutoa nafuu kwa bidhaa za nje
hali inayopelekea viwanda vya ndani kushindwa kushindana na wengine wakabainisha changamoto ya vat
kuwa juu pamoja na malipo ya osha kuwa ni kikwazo kikubwa.
Hali hiyo wameeleza kuwa imewafanya wapate woga kwa
wawekezaji kwa kuhofia kushindwa kufanya biashara nchini na kupelekea nchi
kuendelea kuagiza nguo na vitu mbalimbali kutoka nje ya nchi.
Waziri wa
Nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji,Mhe Angela Kairuki akikagua moja ya kiwanda wakati akifanya ziara ya
kutembelea viwanda mkoani morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...