Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (wa pili kulia) akikabidhi cheti
cha usajili wa Umoja wa Mafundi Simu za Mkononi wa Kanda ya Ziwa kwa
Mwenyekiti wa Umoja huo, Magua Manyanda kwenye Taasisi ya Teknolojia ya
Dar es Salaam, kampasi ya Mwanza. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa
Mawasiliano wa Wizara hiyo, Dkt. Maria Sasabo
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (akiongea na simu ya mezani
iliyotengenezwa na kjwa simu janja (smart phone)) aliyopatiwa na
Mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi Simu za Mkononi wa Kanda ya Ziwa, Magua
Manyanda (aliyeshika kipaza sauti) kabla ya kufungua mafunzo hayo kwenye
kampasi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Mwanza
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (aliyeketi katikati) akiwa kwenye
picha ya pamoja na mafundi simu za mkononi wa Kanda ya Ziwa baada ya
kufungua mafunzo yao kwenye Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Kampasi
ya Mwanza. Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa Mawasiliano wa Wizara hiyo,
Dkt. Maria Sasabo
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania, Mhandisi James Kilaba akiwatunza mafundi simu za
mkononi wa Kanda ya Ziwa wakati wakicheza muziki kumkaribisha Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (anayecheza wa
kwanza mbele) alipowasili kufungua mafunzo yao na kuwapa cheti cha
usaajili kwenye Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Kampasi ya Mwanza
Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania, Mhandisi Francis Mihayo akimpongeza Mwenyekiti
wa Umoja wa Mafundi Simu za Mkononi wa Kanda ya Ziwa, Magua Manyanda,
baada ya kusoma hotuba yake kwa niaba ya Umoja huo kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe alipofika kufungua
mafunzo yao kwenye Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam, Kampasi ya
Mwanza
……………..
Na Prisca Ulomi, Mwanza
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (Mb), amefungua mafunzo kwa mafundi
simu za mkononi wa Kanda ya Ziwa wa kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera,
Mara, Geita, Shinyanga na Simiyu
Kamwelwe amefungua mafunzo hayo
yatakayofanyika kwa mafundi simu za mkononi wa Kanda ya Ziwa wapatao 200
ambayo yamepangwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu kwenye Taasisi ya
Teknolojia ya Dar es Salaam, Kampasi ya Mwanza.
Kamwelwe amewaeleza mafundi simu
za mkononi kuwa wateja watakuwa hawana wasiwasi na wao kwa kuwa watakuwa
wanaleta simu zao kutengenezwa kwa mafundi simu za mkononi ambao
wamepata mafunzo yaliyotolewa na Serikali kupitia wataalamu wa DIT chini
ya uratibu wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania (TCRA) ambao
wamedhamini na kufanikisha uendeshaji na kugharamia mafunzo hayo kwa
Kanda ya Ziwa
“Ninyi ni mafundi ambao mtapata
mafunzo na mtapatiwa miongozo, leseni na mmesajiliwa, mteja anapoleta
simu yake kwako anakuwa hana wasiwasi kwa wizi na kwa wale ambao wanaiba
simu na kuleta kwenu, nalo mtakuwa mmelimaliza kwa kuwa mtawabaini na
kuwashughulikia kwa kushirikiana na mamlaka husika,” amesema Kamwelwe.
Kamwelwe amewataka mafundi simu
kujiunga pamoja ili waweze kupewa leseni na Serikali kutoka TCRA ili
waweze kuitumia kununua vifaa vinavyohitajika kutengenezea simu ya
mkononi na vifaa vingine vya TEHAMA ambavyo vitakuwa vimeharibika na
vinahitaji kufanyiwa matengenezo ambapo amewaeleza mafundi hao kuwa kama
hawana mtaji wamuone
Pia, ameongeza kuwa Serikali
kupitia TCRA imeamua kuwajengea uwezo mafundi simu za mkononi ili kuweza
kuwahudumia watanzania takribani milioni 34 wanaomiliki simu za mkononi
na Serikali haiku tayari kuleta mafundi simu kutoka nje ya Taanzania
ili kupitia mafunzo tuendelee kutoa ajira kwa vijana na tutaendelea
kuwaweka kwenye vikundi maalumu ili muweze kusaidiwa kisheria kama
ilivyo leo kwa kuwapatia mafunzo
Akizungumza wakati wa kumkaribisha
Kamwelwe, Katibu Mkuu wa Mawasiliano wa Wizara hiyo, Dkt. Maria Sasabo
amewaeleza mafundi simu za mkononi kuwa nae ni fundi kwa kuwa alisoma
DIT akawa fundi mchundo ambapo amewahimiza mafundi hao na kuwatia moyo
kuwa washirikiane vema na mafundi simu wa kike ambao wanapatiwa mafunzo
na kuwaomba wakufunzi kuhakikisha kuwa wanawasaidia mafundi simu wa kike
kushiriki kikamilifu na kuhitimu mafunzo hayo
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TCRA,
Mhandisi James Kilaba amewaeleza mafundi hao kuwa wayape kipaumbele
mafunzo hayo kwa kuwa masuala mbali mbali yatafundishwa ikiwemo
ujasiriamali ili kurasimisha mafunzo na ufundi kwa mafundi simu ili
kuchochea ukuaji na ongezeko la la watumiaji wa vifaa vya huduma za
mawasiliano na simu za mkononi
Kilaba ameongeza kuwa usalama na
ubora wa vifaa vya mawasiliano ni jukumu letu sote ambapo mafundi simu
ni sehemu ya utekelezaji na mafunzo haya yataendelea kutolewa na TCRA
kwenye ofisi zake ikiwemo kwenye ofisi ya Kanda ya Kati ambapo amfunzo
yatafanyika Dodoma, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya), Kanda ya
Kaskazini (Arusha) na Kanda ya Zanzibar (Unguja)
Mkuu wa Mafunzo wa DIT, kampasi ya
Mwanza, Dkt. Albert Mmari amesema kuwa DIT ilitoa mafunzo kama hayo kwa
mafundi simu za mkononi wa Dar es Salaam katika kipindi cha mwaka mmoja
na nusu uliopita na sasa wamejiandaa kutoa mafunzo hayo Mwanza kwa
mafundi hao wa Kanda ya Ziwa
Mmari amewaomba mafundi hao
kuhudhuria mafunzo hayo na washirikiane na TCRA kuwaelemisha wadau na
wateja kupeleka simu zao za mkononi kwa mafundi simu waliopata mafunzo
ili kulinda usalama na ubora wa simu zao na vifaa vingine vya TEHAMA
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa
Mafundi Simu za Mkononi wa Kanda ya Ziwa, Magua Manyanda amemshukuru
Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa TCRA, Mhandisi Francis Mihayo kwa kuwakutanisha
mafundi hao, kuwaweka pamoja, kusimamia uanzishwaji wa umoja wao na
kuwaandalia mafunzo ili waweze kushirikiana na Serikali na mamlaka
nyingine kudhibiti uhalifu unaosababishwa na simu za mkononi ambapo
mafundi simu wako tayari kushirikiana na TCRA na Jeshi la Polisi
kudhibiti wezi wa simu za mkononi na kupitia umoja huo, kwa fundi simu
atakayebainika kushirikiana na wahalifu na genge la wezi ataondolewa
mara moja kwenye umoja huo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...