Meneja wa Uwezo Tanzania Zaida
Mgalla akizungumza na washiriki hawapo pichani wa mdahalo wa uwajibikaji
wa pamoja katika kuleta elimu bora na jumuishi katika manispaa ya
Ubungo uliowashirikisha wazazi, walimu, wanafunzi, viongozi wa dini
pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali za mitaa pamoja na wadau wa
maendeleo katika sekta ya elimu.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Afisa elimu vifaa na Takwimu
katika Manispaa ya Ubungo Brayson Maleko akizungumza na waandishi wa
habari hawapo pichani kuhusina na mikakati ambayo wamejiwekea katika
kusaidia na kuinua sekta ya elimu ikiwemo kuanzisha kampeni ya kuondoa
vitendo vya ukatili kwa watoto wa mashuleni.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

\Mmoja wa walimu kutoka shule ya
msingi Goba iliyopo katika Manispaa ua Ubungo Ambrose Mbwala ambaye
alishiriki katika mdahalo huo akitoa ufafanuzi juu ya changamoto ambazo
zinapelekea baadhi ya wanafunzi kujiingiza katika mambo ambayo hayana
faida kwa jamii (PICHA NA VICTOR MASANGU)

Baadhi ya wakufunzi wa mdahalo
huo wakiwa wanafuatili mdahalo ulioandaliwa na shirika la OCODE
kuhusiana na suala zima la elimu jumuishi na elimu bora katika maeneo
mbali mbali hususan kwa wanafunzi wa shule za msingi katika manispaa ya
Ubungo.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Walimu kutoka shule tofauti za
msingi wakiwa wanafuatilia mwenendo mzima wa mhadalo huo ukiendelea
katika maeneo ya Kiluvya madukani wenye lengo la kujadili mambo
yanayohusina na sekta ya elimu jumuishi hasa kwa watoto wa shule za
msingi.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
……………………………………………..
VICTOR MASANGU, UBUNGO
KATIKA kuunga mkono juhudi za
serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini
hususan kwa wanafunzi wa shule za msingi hasa kwa wale wenye mahitaji
maalumu Shirika la Organization for Community Development (OCODE)
limeamua kuja na mpango wa kutoa mafunzo kwa walimu, wanafunzi na wazazi
kuhusiana na umuhimu wa elimu bora na elimu jumuishi pamoja na
kujadili changamoto zilizopo ili kuzitafutia ufumbuzi.
Hayo yamebainishwa na Afisa
miradi kutoka shirika hilo la OCODE Tunu Sanga wakati wa mdahalo wa
uwajibikaji wa pamoja katika kuleta elimu bora na jumuishi lengo ikiwa
ni kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi wanapata haki yao ya
upatikanaji wa elimu iliyo bora kwa ajili ya kuleta mabadilik chanya ya
kimaendeleo katika siku zijazo.
Aidha alisema kwamba lengo kubwa
la Shirika lao ni kushirkiana na wadau mbali mbali wa sekta ya elimu
kukaa pamoja na kujadili mambo mbali mbali ambayo yatasaidia kwa kiasi
kikubwa katika mfumo mzima wa kuwa na elimu jumuishi na elimu iliyobora
hasa katika makundi ya watu wenye ulemavu na wale wenye mahitaji
maalumu.
“Tupo katika mdahalo huu
ambao tumeamua kuuandaa kwa kushirikiana na watu mbali mbali wakiwemo
viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa, walimu, wazazi, pamoja
na wanafunzi ili tuone ni namna gani tunaweza kufika mbali katika suala
zima la kuwa na elimu jumuishi hivyo kwa sasa tupo katika manispaa ya
ubungo na kwamba tutaendelea katika maeneo mengine ya Jiji la Dar es
Salaam,”alisema Sanga.
Kwa upande wake Afisa elimu
vifaa na Takwimu katika Manispaa ya Ubungo Brayson Maleko amebainisha
kwamba kwa sasa kumekuwepo na matukio mbali mbali ya vitendo vya
kikatili na unyanyasaji kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi
kulawitiwa kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo wazazi na walezi kuwa
na malezi mabaya kwa watoto wao.
Pia katika kupambana na hali hiyo
kwa sasa Manispaa ya ubongo imeanzisha kampeni maalumu kwa ajili ya
kupita katika kata zote 14 lengo ikiwani ni kutoa elimu pamoja na
kukataa na kupinga kabisa vitendo vya mtoto wa kiume kulawitiwa kwani ni
kinyume kabisa na sheri na taratibu za nchi zilizowekwa na kuwaasa
wazazi kuhakikisha wanalisimaamia kwa pamoja suala hilo lisiweze
kujitokeza tena.
“Ndugu mwandishi kwa sasa
wanafunzi wa kiume wapatao 12 katika shule moja ya msingi iliyopo
iliyopo katika Manispaa ya Ubungo Jijini Dar e es Salaam wamebainika
kufanyiwa vitendo vya ukatili ikiwemo kulawitiwa na wazazi wao na
wengine kulawitiana wenyewe kwa wenyewe kutokana na sababu mbali mbali
ya ukosefu wa elimu pamoja na malezi mabaya kutoka kwa wazazi wao na
walezi,”alisema Maleko.
Kwa upande wake Meneja wa Uwezo
Tanzania Zaida Mgalla aliwaasa wazazi na walezi kuhakikisha
wanawalinda na kuwatunza watoto wao ili waweze kujitambua na kuepukana
na vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuwataka walimu kuwa na nidhamu,
huku mmoja wa walimu walioshiriki katika Mdahalo huo Ambrose Mbwala
amesema kuwepo kwa baadhi ya wanafunzi kufanyiwa ulawiti vinatokana
na tabia ya kushiriki mambo mabaya ya mitani ikiwemo, ngoma,utandawazi,
pamoja na vigodoro vya usiku.
MDAHALO huo umewajumjisha wadau
mbali mbali wa sekta ya elimu, viongozi wa dini,viongozi wa serikali za
mitaa, wazazi, wanafunzi, pamoja na walimu kwa lengo la kuweza
kuhakikisha elimu bora na elimu jumuishi katika ngazi za shule za msingi
ili kuweza kuboresha sekta ya elimu kwa kushirikiana na serikali ya
awamu ya tano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...