Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akihutubia kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge hivi karibuni.

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani hivi karibuni.
………………………………………………
NA TIGANYA VINCENT
MADIWANI na Viongozi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge wametakiwa kuachana na mpango
waliokusudia wa kutenga Kituo cha ukusanyaji wa asali bali wafikirie
wazo la ujenzi wa Kiwanda cha kusindika asali ili kuongeza thamani ya
asali hiyo.
Ushauri huo umetolewa juzi wilayani Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.
Alisema utaratibu wa ujenzi wa
Kiwanda utawasaidia wafugaji wa nyuki kupata faida kubwa na kuwa na
bidhaa ambazo zinajulukiana asili yake zinazalishwa na Kiwanda cha
Sikonge(Made in Sikonge)
Mwanri alisema kitendo cha
kuruhusu Sikonge kugeuka kuwa sehemu ya kukusanya asali ambayo
haijasindikwa utasababisha watu kutoka nje kuingia katika eneo la
kukusanya asali yote na kuwaacha wafugaji wakiwa na faida kidogo huko
ikienda kunufaisha maeneo mengine.
“ Naona Sikonge hatuelewani mimi
nazungumzia uanzishaji wa Kiwanda cha kusindika asali na kuiweka kwenye
vifungashio kama vile Chupa ambazo zina nembo ya Sikonge, nyie
mnafikiria kuwa na ‘collection centre’ ambapo asali itauzwa kabla ya
kuongezewa thamani na kwenda kunufaisha watu wa sehemu nyingine na
kuwacha watu wakiwa maskini “ alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...