Afisa Utumishi Ofisi ya Makamu wa Rais ya Zanzibar Bakari Maulid Bakari (wa pili kushoto) akitoa maelezo kuhusu shughuli za ofisi hiyo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George
Simbachawene. Wengine kushoto ni Mhasibu Mohamed said Mwinyi na kulia ni Mratibu Othman Haji.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akiagana na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Tunguu, Zanzibar kabla ya kuelekea Pemba kwa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akipokewa na Mratibu wa shughuli za Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Othman Kassim Haji mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Makamu wa Rais zilizopo Tunguu, Zanzibar ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo Pemba.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Tunguu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene (katikati) akiongozwa na Afisa Utumishi, Bakari Maulid Bakari (kulia) kutembelea Ofisi za Makamu wa Rais zilizopo Tunguu, Zanzibar ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo Pemba. Kushoto ni Mhasibu kutoka Ofisi hiyo Mohamed Said Mwinyi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...