Wenyeji wa Mkoa wa Kilimanjaro watakaoenda likizo mwaka huu kwa msimu wa sikukukuu wameandaliwa burudani mbalimbali kwenye Tamasha  kubwa linalotarajiwa kufanyika  tarehe 22 Disemba 2019 kwenye Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi.

Tamasha hilo linalojulikana kama ‘Twenzetu Kilimanjaro Fest’ 2019 limendaliwa na Kampuni ya Real PR Solutions ya jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia Tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuzinduliwa rasmi hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo Bw Clement Mshana amesema ni sehemu ya mkakati wa kufanikisha Mpango wa Kuendeleza Utalii wa Ndani (Domestic Tourism Promotion Initiative (DTPI) unaotarajiwa kufanyika mikoa mbalimbali nchi nzima kwa kuanza  na Mkoa wa Kilimanjaro.
“Tamasha hili la Twenzetu Kilimanjaro Fest  linatarajiwa kupambwa na matukio kadhaa ya burudani zikiwemo, Mbio za kujifurahisha za Capital Mountain Run zitakazohusisha Km 5, Km 10 pamoja na mbio za watoto za Km 3 na Mbio za Baiskeli za KM 60, Maonesho ya Utalii na Biashara, Burudani na viburudisho mbalimbali ikiwemo michezo ya watoto, vyakula vya asili na muziki.’’ Alitaja.
Alisema katika Mkoa wa Kilimanjaro Tamasha hilo hasa litahusisha agenda kuu tatu ambazo ni pamoja na kutangaza Utalii wa ndani, upandaji wa miti  pamoja na kuhamasisha uwekezaji wa viwanda katika mkoa huo.
Aidha katika mkakati wake wa kufanikisha agenda hizo, kampuni hiyo ya Real Pr Solutions imeandaa matukio kadhaa ya kijamii ili kuunganisha wadau mbalimbali wa mkoa huo kama utembeleaji wa vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo mkoani Kilimanjaro ikiwemo, Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi na maporomoko mbalimbali ya maji yaliyopo mkoani humo.
“Tutukio hili la  utembeleaji wa vivutio na upandaji miti linatarajiwa kufanyika Disemba 21, 2019 yaani siku moja kabla ya Tamasha,’’ alisema huku akitaja tukio jingine kuwa ni upandaji wa miti zoezi ambalo litatekelezwa kwa uratibu wa pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) likihusisha wadau mbalimbali ikiwemo mashirika na taasisi za umma ikiwemo shule na vyuo mbalimbali mkoani Kilimanjaro.
Mbali na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)aliwataja baadhi ya wadau muhimu katika ufanikisha tamasha hilo kuwa ni pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
“ Wengine ni pamoja na Kampuni ya Ujenzi ya CRJE (East Africa) Limited, HAL, Kilimanjaro Wonders Hotel, Nyumbani Hotels na Afrimax Strategic Partnerships.”
 “Kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya Tamasha hili ninawaomba sana wadau mbalimbali wajitokeze kutuunga mkono ili tuweze kufanikisha maandalizi ya Utekelezaji wa Mpango huo.’’ Alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...