WAKAZI wa
Halmashauri ya Wilaya ya Tabora(Uyui) wanatarajia kulima hekta 5,000 za zao la
pamba katika msimu wa kilimo unaoendelea mkoani Tabora.
Kauli hiyo
imetolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati akitoa taarifa ya
kilimo cha zao hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora alipotembelea Wilaya hiyo
kuhamasisha shughuli za kilimo.
Alisema kutokana na
makadirio hayo wanatarajia kuzalisha tani 3,500 za zao hilo katika mavuno
yajayo.
Msuya alisema jumla
ya vyama msingi nane vimeshapokea mbegu na ugawaji kwa wakulima mbalimbali
unaendelea.Mkuu huyo wa Wilaya
alisema katika msimu uliopita walilenga kulima hekta 4,000 lakini walifanikiwa
kulima hekta 1,700 na kuwafanikiwa kuzalisha kilo milioni 1.2.
Alisema katika kilo
hizo wakulima walipwa shilingi milioni 1.5 ambapo wakulima wameshalipwa na
Kampuni ya KCCL na KOM.Aidha alisema hadi
hivi sasa Vyama vya Msingi vinadaiwa shilingi milioni 53.4 ikiwa ni gharama za
mbegu na pembejeo.
Msuya alisema wamewaagiza
Watendaji wa Vijiji kushirikiana na Askari wa Akiba kuhakikisha wanawabaini
wale wote ambao wamechukua pembejeo na hawakulima na wale waliotorosha pamba
yao ili waweze kulipa madeni yao.
Kwa upande wa Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliwaagiza viongozi mbalimbali wa kuanzia ngazi
ya Kijiji hadi Kata kulima kitaalamu ekari tatu za pamba ili kuwahamasisha
wananchi wengi kushiriki katika kilimo hicho.
Alisema hatua hiyo
itaisaidia Halmashauri yao kupata ushuru mwingi unaotokana na mauzo ya pamba
ikiwa ni sehemu ya kuongeza mapato yake ya ndani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...