Na.Khadija seif, Michuzi TV
MLEZI
wa kituo cha kulea watoto yatima cha kurasini Bi.Anna amewaomba wazazi
kuiona fursa ya kusaidia watoto waishio kwenye mazingira magumu
Bi.Anna
amesema hayo wakati wa sherehe ya kukaribisha sikukuu ya krismas
iliyoandaliwa na hoteli ya serena jijini Dar es salaam na kujumuisha
watoto yatima kutoka vituo mbalimbali .
"Watoto
hawa ni wetu sote jukumu la kuwalea sio la serikali au watu binafsi
peke yao bali ni jukumu la Kila mtanzania kwani tukiwaacha
tunawatengenezea mazingira hatarishi na kupelekea kujiingiza kwenye
vitendo viovu vya ubakaji,ukahaba pamoja wizi na kusababisha nchi kuwa
na watu waovu wengi na kurudisha maendeleo ya jamii yetu kuzorota"
Aidha,mama
mlezi wa watoto ameeleza changamoto anazopitia katika ukuaji wao hasa
wale walemavu ni pamoja na kukosa vifaa vinavyowawezesha kufanya
mawasiliano ya usiku kwa viziwi, na baiskeli kwa watoto walemavu wa
miguu.
"Kuelekea sikukuu
ya Christmas na sikukuu nyingine watu wamekua wakija kituoni na
kuwapatia misaada mbalimbali watoto wetu kuonyesha upendo na jinsi gani
wanawathamini watoto ,"
Pia
amewapongeza uongozi wa hoteli ya serena kwa kuendelea kuonyesha upendo
wa dhati kila mwaka na kuwakaribisha watoto na kucheza,kujumuika kwenye
chakula pamoja nao.
''watoto
wanapokutana na kushiriki michezo inawajengea uwezo wa kujiamini mbele
za watu na pia inatupa uhalisia kuwa hata wao wanavipaji vingi na hasa
leo tumeona wengi wanajua kuimba na kucheza,"
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...