Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Dkt.Sophia Mlote  ametoa wiki mbili kwa wachuuzi wa maziwa eneo la ubungo kutafuta eneo rasmi la kuendesha biashara ya maziwa kwani eneo linalotumika kwa sasa linahatarisha usalama wa maziwa kwa afya ya mlaji.

Hayo alisema leo (16.12.2019) wakati wa zoezi la ukaguzi wa ubora wa maziwa liloambatana na utoaji wa elimu kwa wadau katika eneo maarufu la uuzaji wa maziwa la ubungo jijini Dar es Salaam.

Dkt.Mlote amesema eneo hilo halijasajiliwa na Bodi na si salama kwa uendeshaji wa biashara maziwa kwa mujibu wa kanuni na sheria ya maziwa ya mwaka (2004).

Dkt.Mlote amesema ujenzi unaoendelea katika eneo la ubungo sambamba na uchafu wa mazingira katika eneo hilo unahatarisha usalama wa maziwa kwa mlaji na hivyo kuwataka wachuuzi hao kutafuta mbadala wa eneo lingine kwa ajili ya uendeshaji wa biashara ya maziwa.

"Natoa wiki mbili mtafute mahali tupasajili"  alisema

Aidha, Dkt Mlote ametoa katazo la matumizi ya vyombo vya plastic katika kuhifadhi maziwa kwani vyombo hivyo hufanya uchafuzi wa maziwa na kuhatarisha afya ya mlaji.

Dkt Mlote amewataka wachuuzi hao kutumia vyombo vinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria katika kutunzia maziwa ambavyo ni metaliki na aluminiamu.

Katika zoezi hilo bodi ya maziwa iliweza kubaini uuzwaji holela wa maziwa usiofuata sheria na kanuni na hivyo kutoa elimu kwa wadau kuhusu sheria ya maziwa ikiwemo usajili wa wadau.
Afisa Usindikaji wa Bodi ya Maziwa  Emmanuel Mushi akitoa elimu ya upimaji wa ubora wa maziwa kwa wachuuzi wa maziwa leo maeneo ya ubungo.


Baadhi ya wachuuzi wa Maziwa eneo la Ubungo
Wachuuzi wa Maziwa eneo la Ubungo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...