Bi Godfrida Mwashitete  mkazi wa Kijiji cha Ikumbilo Ileje akiwa njiani kurudi kwake baada ya kupata msamaha wa Rais.
 Baada ya kuachiwa huru kwa msamaha wa Rais katika gereza la Ileje raia hawa wakijiandaa kurudi makwao ili kuungana na  familia zao.
 Mkuu wa Wilaya ya Ileje Ndg. Joseph Mkude aliyevaa suti ya bluu na tai nyekundunda akizungumza na waliopata msamaha wa Rais akisisitiza maagizo ya r
Waliokuwa wafungwa katika Gereza la Ileje wakisubiri kurusiwa kurudi kwao baada ya kupata msamaha wa Rais 2019.

Na Daniel Mwambene Ileje

Wafungwa 15 Wilayani Ileje mkoani Songwe wamenufaika na msamaha wa Rais alioutoa wakati wa sherehe za Uhuru 2019 huku Mkuu wa Wilaya akiwataka kuzingatia maagizo ya Mhe.Rais Magufuli.

Ikiwa ni asubuhi tulivu iliyojaa mawingu yanayodondosha matone madogomadogo jumla ya wafungwa 15 wakiwemo wanaume 14 na mwanamke mmoja wamejikuta wakiachiwa huru mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo akiwa na Kamati ya Ulinzi pamoja na vyombo vya habari.

Tukio hilo lililofanyika ukiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuwachia wafungwa waliokuwa na sifa ili kurudi uraiani kuunganana na jama zao.

“Msiende kuwa wanyonge kwasababu mmetoka gerezani,nendeni mkapambane na maisha na kuhakikisha kuwa mnainua hali zenu na kuwa mfano wa kuigwa na jamii”alisisitiza Ndg.Joseph Mkude Mkuu wa Wilaya ya Ileje.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hiz wakiwa njiani kuelekea makwao baadhi yao waliipongeza serikali kwa kufanya hivyo wakiahidi kwenda kuwa raia wema.

Godfrida Mwashitete mwanamke pekee aliyeachiwa siku hiyo alisema kuwa,katika maisha haitakiwi kurahisisha mambo kwa kuvunja sheria hali aliyoielezea kuwa mkono wake ukikupitia unaweza kufungwa na kujikuta unaachana na maisha ya uhuru.

Aliongeza kuwa anamshukuru Rais na watendaji wake wote waliofanikisha yeye kuachiwa ili akaungane na familia yake aliyoachana nayo kwa takribani mwaka mzima.
Shida Mbughi alifurahia kuachiwa akimpongeza Mhe.Rais kwakuwa hakutegemea kuwa msamaha kama huo ungemwangukia yeye pia akisema anaenda kuwa raia mwema.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...